Pata taarifa kuu
CAR-UN-USALAMA

Suala la kuondoa vikwazo vya silaha lajadiliwa CAR

Waziri wa Ulinzi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Joseph Yakété, ametoa taarifa kuhusu "mazungumzo" na Umoja wa Mataifa kwa lengo la kuondoa vikwazo vya silaha katika hali ya kuboresha jeshi la kawaida nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ambapo hali ya usalama bado ni tete.

Askari polisi wakitoa ulinzi katika kituo cha kuhesabu kura za uchaguzi wa urais na ubunge mjini Bangui, Januari 2, 2016.
Askari polisi wakitoa ulinzi katika kituo cha kuhesabu kura za uchaguzi wa urais na ubunge mjini Bangui, Januari 2, 2016. SSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Vikwazo hivyo vya silaha vilivyowekwa mwaka 2013, viliongezewa muda wa mwaka mmoja na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa mwezi Januari. Kwa upande wa serikali wanasema, kuondolewa kwa vikwazo hivi ni muhimu na itapelekea kuimarika kwa jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Idadi ya jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati sasa imefikia 7,500, na kwa mujibu wa vyanzo kadhaa ni robo tu ya askari hao ambayo wana silaha. Kwa upande wa serikali ya Jamhuri ya Afrika ya Kati wanasema, lengo la kwanza ni kupata silaha zinazohifadhiwa katika nchi jirani, ikiwa ni pamoja na Cameroon, tangu kuwasili kwa kundi la waasi wa zamani wa Seleka katika mji wa Bangui, akati askari wa Jamhuri ya Afrika ya Kati walipovuka mipaka, wakiwa na silaha zao.

Lengo la pili: kupata fedha kwa ajili ya mipango ya vifaa. Si tu kwa silaha lakini pia sare, magari, rvifaa vya mawasiliano na vifaa vingine vya kijeshi.

Kuna utaratibu kuondoa vikwazo lakini moja kwa moja. "Umoja wa Mataifa bado unatazama kwa makini suala hili," chanzo cha kuaminika kimesema. Hivi karibuni Ufaransa umelipatishi jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati baadhi ya vifaa vya jeshi hasa vile vya kujilinda na risasi.

Kwa suala la kuondoa vikwazo vya silaha, ni mchakato mrefu. "Tutakuwa na kutoa dhamana kwa jumuiya ya kimataifa kuhusu masharti ya uhifadhi wa silaha kwa mfano, kuhusu mageuzi ya vikosi vya jeshi pia" chanzo cha kijeshi kimeeleza. "Ili kuimarisha usalama, FACA (jeshi la Jamhuri ya Afrika ya Kati) linapaswa kupewa mafunzo, kupatishiwa vifaa na kupewa mafunzo ya kivita, " chanzo kingine cha serikali kimebaini. "Ni jukumu la jeshi na kwa kuwa tunahitaji vikwazo viondolewe angalau vipunguzwe kwa haraka iwezekanavyo. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.