Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Kampeni za kisiasa zapigwa marufuku nchini Zambia

Kampeni za kisiasa nchini Zambia kuelekea uchaguzi Mkuu tarehe 11 mwezi ujao zimesitishwa kwa sababu ya kuongezeka kwa visa vya machafuko ya kisiasa.

Rais Edgar Lungu akiwa kwenye mkutano wa kisiasa hivi karibuni
Rais Edgar Lungu akiwa kwenye mkutano wa kisiasa hivi karibuni cdn.mg.co.za
Matangazo ya kibiashara

Tume ya Uchaguzi nchini humo imesema kuwa imesitisha kampeni hizo kwa muda wa siku 10 zijazo kuanzia mwishoni mwa juma hili.

Ripoti kutoka Zambia zinasema wafuasi wa chama tawala cha PF cha rais Edgar Lungu ambaye anatetea wadhifa wake, wamekuwa wakipambana na wale kiongozi wa upinzani wa chama cha UPND kinachoongozwa na Hakainde Hichilema.

Siku ya Juma, polisi walitumia nguvu dhidi ya wafuasi wa upinzani jijini Lusaka na kumuua mtu mmoja baada ya chama cha upinzani UPND kukata kusitisha mkutano wake wa kampeni.

Msemaji wa Tume hiyo Cris Akufuna amesema mikutano ya nyumba kwa nyumba au mikutano yoyote haitaruhusiwa kwa muda huo wa siku 10.

Upinzani umeishtumu serikali kwa kutumia polisi kuwanyima vibali vya kuendelea na mikutano yake na badala yake kuipendelea serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.