Pata taarifa kuu
ZAMBIA

Serikali: Hatuhusiki na kufungwa kwa gazeti la The Post

Juma moja baada ya kufungwa kwa gazeti maarufu la kila siku nchini Zambia la “The Post” kwa tuhuma za kukwepa kulipa kodi, jana jioni Polisi mjini Lusaka wamemkamata mmoja wa wahariri wakuu wa gazeti hilo.

Nakala ya gazeti la The Post kwenye mtandao, ambalo limefungiwa na Serikali juma moja lililopita.
Nakala ya gazeti la The Post kwenye mtandao, ambalo limefungiwa na Serikali juma moja lililopita. RFI
Matangazo ya kibiashara

Mhariri mkuu na naibu wake, walikamatwa wakiwa nje ya ofisi za gazeti hilo ambazo zimeendelea kufungwa, huku hadi sasa Polisi wakiwa hawajawafungulia mashtaka ya aina yoyote kuhusiana na kile kilichotokea.

Gazeti hilo linakanusha madai ya mamlaka ya mapato nchini humo kuwa linadaiwa mamilioni ya pesa, na badala yake linasema ukosoaji wake dhidi ya Serikali ndio ulioifanya Serikali kuiagiza mamlaka ya mapato kuzifunga ofisi zake.

Hata hivyo madai haya yanakanushwa vikali na msemaji wa rais Edgar Lungu, AMOS CHANDA, ambaye anasema Serikali haina ugomvi wowote na gazeti hilo kwakuwa limekuwa likichapisha habari za kuikosoa serikali kwa miaka 25 iliyopita, na kwamba ikiwa litalipa kodi linazodaiwa, mamlaka ya mapato haitasita kurejesha mali zake na kulifungua.

Juma hili pia Serikali ya Marekani imetoa wito kwa Serikali na vyombo vingine husika nchini Zambia kuzifungua ofisi za gazeti hilo, kwa kile ilichosema inaguswa na namna uhuru wa vyombo vya habari unavyoingiliwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.