Pata taarifa kuu
KENYA

CORD yaipa Serikali hadi kufikia Jumatano kutimiza matakwa yao

Muungano wa upinzani nchini Kenya, CORD, umeahirisha maandamano yake ya kila Jumatatu kushinikiza kujiuzulu kwa makamishna wa Tume ya Uchaguzi IEBC.  

Mfuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya wa Cord akiwa amebeba bango kuikoso IEBC
Mfuasi wa muungano wa upinzani nchini Kenya wa Cord akiwa amebeba bango kuikoso IEBC REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Wanasiasa wakuu wa muungano huo seneta, James Orengo na Johnston Muthama, wamesema maandamano hayo hayatafanyika leo kutoa nafasi kwa mazungumzo ya kuelekea kupata mwafaka wa pande zote kuanza mazungumzo.

Hata hivyo, CORD imesema itarejelea maandamano yake siku ya Alhamisi wiki hii ikiwa kufikia saa 3 usiku siku ya Jumatano upande wa serikali hautakuwa umekubali matakwa yao ya kutaka mazungumzo yafanyike nje ya bunge na kupunguza idadi ya wajumbe wake kufikia wanne.

Mwishoni mwa wiki iliyopita, viongozi wa upinzani walikutana na viongozi wa dini ambao ni wasuluhishi katika mzozo huu, wafanyibiashara na wanadiplomasia kujadiliana kwa kina kuhusu mazungumzo haya.

Rais Uhuru Kenyatta ameendelea kusisitiza kuwa mazungumzo hayo ni lazima yafuate sheria na kufanyika ndani ya bunge chini ya kamati maalum, na wiki iliyopita alitangaza wajumbe 11kuiwakilisha serikali.

Hata hivyo, kiongozi wa CORD Raila Odinga amesema ni sharti mazungumzo hayo yafanyike nje ya bunge kisha baadaye kupitishwa na wabunge kwa madai kuwa wabunge wa serikali ni wengi na wanaweza kutumia wingi wao kupinga maafikiano yoyote kuhusu mageuzi kuhusu tume ya uchaguzi kuelekea uchaguzi Mkuu mwaka ujao

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.