Pata taarifa kuu
MALAWI-AMNESTY

Amnesty International yainyooshea kidole polisi ya Malawi

Shirika la Kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty international linashtumu polisi nchini Malawi kwa kushindwa kuwalinda watu wanaoishi na ulemavu wa ngozi, Albino.

Vijana wa Burundi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) mkoani Ruyigi,Februari 27, 2009.
Vijana wa Burundi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) mkoani Ruyigi,Februari 27, 2009. (Photo : Stéphane Sakutin/AFP)
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, polisi wanasema wamekuwa wakifanya kila kilicho ndani ya uwezo wao kuwalinda watu hao.

Deprose Muchena,Mkuu wa Amnesty International Kusini mwa Afrika amesema Albino nchini Malawi wameachwa kupambana na watu wanaovamia.

Tangu mwaka 2014, Albino 18 wameuawa na wavamizi kutoroka na viungo vya miiili yao kutumia kwa imani za kishirikina.

Visa vya mauaji ya Albino vimekithiri katika nchi mbalimbali barani Afrika. Miaka iliyopita visa hivyo vilishuhudiwa katika nchi za Burundi, Kenya, Tanzania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.