Pata taarifa kuu
CHAD-HABRE

Hissène Habré asubiri kujua hatima yake

Mahakama maalum ya Afrika iliokuwa inasikiliza kesi ya rais wa zamani wa Tchad Hisssene Habre inatarajiwa kutowa hukumu yake baadae hii leo jumatatu baada ya kusikiliza kesi hiyo ambayo inachukuliwa na wengi huenda ikawa mfano kwa bara la Afrika ikiwa ni muongo mmoja baada ya kuanguka kwa utawala wake.

Rais wa zamani wa Chad Hissène Habré, wakati waziara yake Paris Paris, Oktoba 21, 1989.
Rais wa zamani wa Chad Hissène Habré, wakati waziara yake Paris Paris, Oktoba 21, 1989. AFP PHOTO / PATRICK HERTZOG
Matangazo ya kibiashara

Hissene Habre anatuhumiwa makosa ya kivita, unyanyasaji na aliwahi kuliongoza taifa la Tchad kwa kipindi cha miaka 8 kuanzia mwaka 1982 – 1990 kabla ya kupinduliwa na mmoja miongoni mwa washirika wake ambae ni rais wa sasa Idriss Deby Itno ambapo baadae alitumkia nchini Senegal Desemba mwaka 1990 na kuomba hifadhi ya ukimbizi.

Mbaye Sene, anaona Wakili mtetezi wa Hissen Habre anaona kwamba mteja wake atasafoshwa na kuachiwa huru.

Hata hivyo wakili mtetezi wa waathirika jacqueline Moudeina anaona kwamba kifungo kinachomstahili Hissene Habre ni kifungo cha maisha.

Upande wake mwanasheria kutoka shirika linalo tetea wahanga wa vitendo vya unyanyasaji Clemant Abaifouta anasema iwapo habre atapatikana hana hatia basi itakuwa ni kupingana na sheria.

Habre alikamtwa Juni 30 mwaka 2013 na kesi yake imeanza kusikilizwa tangu Julai mwaka 2015 na mahakama maalum ya Afrika iliowekwa kufuatia makubaliano ya Umoja wa Afrika na Senegal na ambayo amekuwa akiipinga na kukataa kujitetea

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.