Pata taarifa kuu

DRC: Moïse Katumbi kuripoti mbele ya mwendesha mashtaka

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, vyombo vya sheria vinataka kumsikiliza Moïse Katumbi. Mkuu wa zamani wa Katanga, alietangaza wiki hii kuwania katika kiti cha urais mwaka huu, ametakiwa kuripoti Jumatatu hii mbele ya mwendesha mashitaka mkuu wa mkoa wa Lubumbashi.

Moïse Katumbi, Lubumbashi, Mei 28.
Moïse Katumbi, Lubumbashi, Mei 28. © AFP PHOTO / FEDERICO SCOPPA
Matangazo ya kibiashara

Hati ya kuripoti Jumatatu, Mei 9 ilipokelewa rasmi Jumamosi Mei 7 asubuhi na wanasheria wa Moïse Katumbi, baada ya masaa kadhaa ya kutatanisha kuhusu hati ya kwanza ya kuripoti siku hiyo.

Tangu Ijumaa wiki iliyopita, hati ya kwanza ya kuripoti ilikua ikisambaa kwenye mitandao ya kijamii. Katika waraka huo, Ofisi ya mashtaka ilimtaka Moïse Katumbi kuripoti Jumamosi saa 4 mchana ili aweze "kusikilizwa juu ya ukweli kwa yale ambayo anatuhumiwa."

Kwa mujibu wa chanzo rasmi katika faili hiyo, mwaliko wa kawaida wa kuhudhuria mara ya kwanza ulitumwa, mwaliko ambao mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga hakuweza kujibu, jambo ambalo lilisababisha kutolewa kwa hati hii ya kuripoti mbele ya mwendesha mashitaka mkuu wa mkoa wa Lubumbashi.

Lakini kwa upande wake, Moïse Katumbi anasema hajapokea mwaliko wowote wala hati ya kumtaka aripoti Jumamosi hii. Bw Katumbi Chapwe aliwatuma wanasheria wake katika Ofisi ya mashtaka Jumamosi asubuhi ili kuthibitisha kuwepo kwa hati ya aina hiyo. Hati ya pili ya kuripoti ilitolewa na Ofisi ya mashitaka mara tu wanasheria wa Moïse Katumbi walipofiki ofisini hapo. Hati ambayo ilimtaka Moïse Katumbi kuripoti Jumatatu hii Mei 9 katika Ofisi kuu ya mashitaka mkoani Lubumbashi saa 4:00 mchana.

Hati hii haielezi bayana kuhusu tuhuma ambazo Moïse Katumbi anakabiliana nazo, lakini tangu Jumatano, Mei 4, uchunguzi ulianzishwa kufuatia ombi la Waziri wa Sheria, aliyemtuhumu mkuu wa zamani wa mkoa wa zamani wa Katanga kuajiri askari mamluki, ikiwa ni pamoja na askari waz amani wa Marekani.

Moïse Katumbi, anasema yuko tayari kuripoti Jumatatu ijayo: "Bila shaka niko chini ya sheria, nitaripoti. Unajua, dhamiri yangu iko sawa, sina hofu yoyote. Sina lolote la kuficha. Na ndio maana niliomba waanzishe uchunguzi, na jumuiya ya kimataifa ishirikishwe katika uchunguzi huo. Mlijionea wenyewe taarifa ya ubalozi wa Marekani. Je, tunaajiri askari mamluki mjini Washington? Kampuni ambayo niliona mjini Washington, ni kampuni inayojulikana. Sina hofu kabisa. Nitakwenda huko. Sina hatia yoyote. "

Jumamosi asubuhi wiki iliyopita polisi iliendesha msako katika moja ya mali zake, shamba linalopatikana kilomita 20 kutoka mji wa Lubumbashi, bila ya uwepo wa Bw Katumbi Chapwe au wanasheria wake. Mkuu wa zamani wa mkoa wa Katanga alishtumu utaratibu uliyotumiwa na polisi akibaini kwamba ni kinyume cha sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.