Pata taarifa kuu
DRC-DEMOKRASIA

DRC: mikutano Kinshasa, makabiliano Lubumbashi

Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, Jumapili hii ilikuwa ni siku ya mikutano. Upinzani na vyama vinavyoshirikiana na chama tawala walisherehekea maadhimisho ya ufunguzi wa mfumo wa kidemokrasia.

Mkutano wa chama cha upinzani mjini Kinshasa, Aprili 24, 2016.
Mkutano wa chama cha upinzani mjini Kinshasa, Aprili 24, 2016. © JUNIOR KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ushindi ulionyakuliwa Aprili 24, 1990 baada ya udikteta uliodumu karibu miongo mitatu. Aprili 24, 1990, katika "Hotuba iliyoashiria demokrasia", Mobutu Sese Seko alitangaza mwisho wa mfumo wa chama kimoja. Katika mji wa Kinshasa, mkutano wa hadhara wa muungano wa vyama vya upinzani ulifanyika kwa amani, lakini katika mji wa Lubumbashi, mkutano wa hadhara ulitawanywa na polisi.

Kulikuwa na hofu zaidi katika mkutano wa muungano wa vyama vya upinzani mjini Kinshasa. Hata hivyo mkutano uliofanyika bila kwa utulivu. Viongozi wa muungano huokila mmoja alipewa nafasi ya kutoa maoni yake, wakikaidi amri ya manispaa ya jiji la Kinshasa ya kufanya mkutano wao katika mahali panapofungwa.

Mkutano uliofanyika kwenye eneo lililo kati ya barabara kuu iliyobatizwa Ushindi ilio karibu na uwanja wa mpira wa Martyrs na mtaa uliobatizwa Elimu. Joseph Olenghankoy, Vital Kamerhe, Fayulu Martin, Jean-Claude Mvuemba na viongozi wengine, kila mmoja amezungumzia kwa siku ya jana, na wote walikumbusha mapambano ya kishujaa ya raia wa Congo ambao wamepelekea ufunguzi wa kisiasa Aprili 24, 1990.

"Tunakataa kurefushwa kwa muhula wa Rais Kabila, tunaomba uchaguzi wa rais na ule wa wabunge ufanyike ndani ya muda uliyowekwa na kikatiba", walisema viongozi hao wa upinzani. Kwa upande wao wamesema, hawakubali mazungumzo yalioanzishwa na Rais Kabila.

Polisi waliokuwepo karibu na eneo la mkutano hawakumsumbua mtu yeyote, na hivyo mkutano huo kumalizika kwa amani. Wakati huo huo vyama vinavyoshirikiana na chama tawala vilifanya mkutano kwa amani kwa kuadhimisha miaka 26 ya mfumo wa vyama vingi nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mkutano huo ulifanyika mbali kidogo, nyumbani kwa mfanyabiashara mmoja mkazio wa Limete.

Maandamano yatawanywa Lubumbashi

Hata hivyo, katika mji wa Lubumbashi, kusini mwa Congo, mkutano wa wanaharakati wa upinzani waliokusanyika kumsikiliza mpinzani Moise Katumbi ulitawanywa na polisi. Mgombea urais amedai kuwa alilengwa wakati huo na risasi zilizorushwa na vikosi vya usalama. Mabomu ya machozi pia yametumiwa kwa kuwatawanya waandamanaji. Timu ya waangalizi kutoka Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu ilizuliwa kuingia sehemi mkutano huo ulikua ukifanyika.

"Tukio ambalo limetokea leo mjini Lubumbashi ni mbaya, kwani mgombea wa kisiasa alizuiliwa kuendesha mkutano wa hadhara," amesikitika Jose Maria Aranaz, mkurugenzi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo .

Lakini msemaji wa serikali Lambert Mende amekanusha madai ya vitisho vilivyovanywa na utawala. Mende amesema, "Polisi ililifanya kazi yake."

"Tulikaza barabara zisifungwi, lakini wao walikua walifunga barabara kwa makusudi, kwa hiyo polisi ililazimika kufungua barabara hizo zilizokua zimefungwa", amesema Lambert Mende.

Icha ya zamani: Etienne Tshisekedi, mwezi Oktoba 2012 Kinshasa.
Icha ya zamani: Etienne Tshisekedi, mwezi Oktoba 2012 Kinshasa. JUNIOR KANNAH / AFP

Wakati huo huo Etienne Tshisekedi, mwanasiasa mkongwe nchini Congo amesema atarejejea nchini mwake katika “siku za hivi karibuni”. Tangazo hili amelitoa katika ujumbe uliorushwa Jumapili hii. Tshisekedi , kiongozi wa kihistoria wa chama cha UDPS, ambaye kwa sasa anaishi Ubelgiji, ameweka wazi msimamo wake : anatarajia kushiriki katika mazungumzo ambayo kwa sasa yanaendeshwa na msuluhishi Edem Kodjo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.