Pata taarifa kuu
DRC-TANZANIA-UBAKAJI-JAMII

Askari 11 wa Tanzania watuhumiwa ubakaji DR Congo

Wasichana 11 na wanawake kadhaa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanadai kuwa walikuwa wajawazito baada ya kunyanyaswa kimapenzi na wanajeshi 11 wa Tanzania wanaolinda amani Mashariki mwa nchi hiyo.

Monusco yakanusha uvumi unaoipaka matope na kuidhalilisha.
Monusco yakanusha uvumi unaoipaka matope na kuidhalilisha. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Kati ya hao 11, wasichana saba wanadai kuwa tayari wamejifungua huku wanne wakisema kuwa bado ni wajawazito.

Umoja wa Mataifa unasema unachunguza ukweli wa madai hayo, dhidi ya wanajeshi hao wa Tanzania wanaolinda amani katika eneo la Mavivi karibu na mji wa Beni.

Visa vya ubakaji kwa wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa vimekithiri. Hivi karibuni wanajeshi kadhaa wa Ujumbe wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (MINUSCA) kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo walirejeshwa nyumbani baada ya kutuhumiwa kuwa walihusika katika visa vya ubakaji nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Hayo yakijiri hali ya usalam inaendelea kudoroa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Mkuu wa jimbo la Kivu ya kaskazini Julien Paluku amesema Serikali ya DRC pamoja na kuendelea kukabiliwa na changamoto ya kiusalama, ina lengo la kukamilisha miradi yake ya maendeleo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.