Pata taarifa kuu
ICC-DRC-BEMBA-SHERIA

ICC yamkuta na hatia Jean-Pierre Bemba

Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita ICC, imemkuta na hatia ya vita vya uhalifu aliyekuwa Makamu wa rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na mwasi Jean-Pierre Bemba.

Jean-Pierre Bemba katika siku ya kwanza ya kesi yake katika mahakama ya kimataifa mjini Hague Novemba 22, 2010.
Jean-Pierre Bemba katika siku ya kwanza ya kesi yake katika mahakama ya kimataifa mjini Hague Novemba 22, 2010. REUTERS/Michael Kooren
Matangazo ya kibiashara

Majaji wa Mahakama hiyo yenye Makao yake mjini Hague nchini Uholanzi wamesema ushahidi umeonesha kuwa Bemba amepatikana na makosa matano ya kihalifu dhidi ya binadamu yaliyotekelezwa na vikosi vyake vya MCL nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, kati ya mwaka 2002 na 2003.

Imeelezwa kuwa Bemba kama kiongozi wa vikosi hivyo, alitoa maagizo kwa wapiganaji wake kuwabaka, kuwauwa na kuwatesa raia nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati wakati alipovituma vikosi hivyo kwenda kusaidia kusitisha mapinduzi dhidi ya rais wa nchi hiyo wakati huop Ange Felix Patasse.

Majaji baada ya ICC wamesema Bemba ataendelea kushikiliwa hadi pale, atakapotangaziwa kifungo hivi karibuni.

Bemba alikamatwa jijini Brussels mwaka 2008 na kukabidhiwa katika Mahakama ya ICC baada kutoroka machafuko jijini Kinshasa mwaka 2007.

Mwaka 2003 alikuwa Makamu wa rais wa DRC baada ya kuwepo kwa mkataba wa amani lakini pia aliwahi kuwa msaidizi binafasi wa kiongozi wa zamani Mobutu Sese Seko.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.