Pata taarifa kuu
SUDANI-USALAMA

Rais Bashir amteuwa kiongozi mpya wa majeshi

Rais wa Sudan, Omar Hassa al-Bashir amemtangaza mkuu mpya wa majeshi wakati huu vikosi vyake vikiendelea kukabiliana na waasi kwenye mji wa Jebel Marra, eneo lililoko magharibi mwa jimbo la Darfur.

Rais wa Sudan Omar Hassan al Bashir
Rais wa Sudan Omar Hassan al Bashir
Matangazo ya kibiashara

Bashir amemteua Luteni Jenerali Emadeddin Adawi kuwa mkuu mpya wa majeshi hatua inayotajwa kama jibu la kumaliza machafuko kwenye eneo la Darfur.

Katika hatua nyingine, licha ya awali rais Bashir kutangaza kuitisha mazungumzo ya kitaifa, upinzani bado unaona kuwa tangazo lake halina nia ya dhati kwakuwa toka alipotangaza hakuna kilichofanyika kutafuta maridhiano ya kitaifa.

Khalid Omer Yousuf kiongozi wa chama cha upinzani nchini Sudan cha SCP amesema mazungumzo ya kitaifa yalioitishwa na rais Bashir ni mchezo wa kisiasa, huwezi kuitisha mazungumzo huku ukiwanyima watu uhuru wa kuzungumza.

Kiongozi huyo amezidi kuwa bado kuna viongozi wapo korokoroni, hivyo rais Bashir angelikuwa na nia nzuri kwanza angeliwaachia huru wafungwa na kuboresha hali halisi ya uwiano wa kitaifa hivyo mazungumzo yanawezekana, vinginevyo bado ni mchezo wa wa kisiasa kuuza sera zake kimataifa.

Wakati huohuo umoja wa mataifa umetoa wito kwa jumuiya ya kimataifa kuongeza misaada zaidi ya kibinadamu, hasa kwa maelfu ya raia wanaokimbia mapigano kwenye jimbo la darfur, eneo ambalo umoja wa Mataifa unasena hali ya kibinadamu inatisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.