Pata taarifa kuu
LIBYA-SERIKALI YA UMOJA

Libya: viongozi hasimu wakutana

Viongozi wa mabaraza mawili ya Bunge hasimu nchini Libya wamekutana Jumanne wiki hii kwa mara ya kwanza jijini Malte, ikiwa ni siku mbili kabla ya kusainiwa kwa mkataba wa kumaliza mvutano baina ya pande hizo mbili chini ya Umoja wa Mataifa unaotarajia kusainiwa nchini Morocco.

Walibya wanaandamana katika mji wa Benghazi dhidi ya pendekezo la Umoja wa Mataifa la serikali ya umoja wa kitaifa, Oktoba 16, 2015.
Walibya wanaandamana katika mji wa Benghazi dhidi ya pendekezo la Umoja wa Mataifa la serikali ya umoja wa kitaifa, Oktoba 16, 2015. AFP PHOTO / ABDULLAH DOMA
Matangazo ya kibiashara

Kituo cha televisheni nchini Libya Annabaa kimewaonyesha Aqila Salah, Spika wa Bunge linalokubalika na Jumuiya ya kimataifa ambalo lilikimbilia mashariki mwa nchi hiyo na Nouri Abou Sahmein Spika wa Bunge lisilokubalika na Jumuiya ya kimataifa lenye makao yake mjini Tripoli, wakipeana salaam wakiwepo pia wajumbe kutoka maubunge hayo mawili pinzani.

Mkutano huu wa kwanza kabisa tangu kutokea mgawanyiko wa kisiasa nchini Libya mwaka 2014 ambapo kuna mabaraza mawili ya bunge na serikali mbili, unakuja ikiwa ni siku mbili kabla ya kusainiwa kwa mkataba wa kumaliza tofauti zao utaosainiwa mjini Shkirat nchini Morocco na viongozi hao wawili. Mkataba huo unaagiza kuunda serikali ya Umoja wa kitaifa.

Katika mkutano wao wa pamoja na waandishi wa habari Abou Sahmein na Salah, wamesisitiza kwamba wanaoenda kusaini mkataba huo chini ya Umoja wa Mataifa, hawajatumwa na mabaraza yao ya bunge, bali watasaini kama wawakilishi wasio rasmi.

Lengo hasa la makubaliano hayo ni kujaribu kurejesha hali ya utulivu nchini Libya, iliotoweka tangu kuanguka kwa utawala wa rais Muamar Gadaffi mwaka 2011.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.