Pata taarifa kuu
UTUUKI-MOROCCO-UGAIDI-USALAMA

Uturuki yawafurusha raia 8 wa Morocco

Alhamisi wiki hii Uturuki imeamuru kufukuza kundi la raia 8 kutoka Morocco ambao walikuwa wakizuiliwa katika uwanja wa ndege wa Istanbul-Ataturk kwa tuhuma za uhusiano na kundi la Islamic State (IS) na kuonya tishio kubwa la wanajihadi walitokea Afrika.

Uturuki imechukua uamzi Alhamisi Novemba 19 wa kuwafukuza raia 8 kutoka Morocco kwa tuhuma za uhusiano na kundi la Islamic State.
Uturuki imechukua uamzi Alhamisi Novemba 19 wa kuwafukuza raia 8 kutoka Morocco kwa tuhuma za uhusiano na kundi la Islamic State. REUTERS/Murad Sezer/Photo d'archives
Matangazo ya kibiashara

Raia hao 8 kutoka Morocco waliowasili Jumanne wiki hii katika uwanja wa ndege wa Uturuki, wakitokea Casablanca, walisema walikua na nia ya kufanya likizo katika mji wa Istanbul. Wamekua wakizuiliwa katika majengo ya Idara ya uhamiaji na kuhojiwa na wataalamu katika masuala ya ukaguzi, ambaowachukuliwa kwamba walikuwa penginewanamgambo wa kiislam, vyanzo vilio karibu na serikali vimebaini.

Uturuki, ambayo mpaka wake na Syria kuna urefu wa kilomita 900 km, ni eneo muhimu la kuingilia kwa wanajihadi wakitokea Ulaya na Afrika Kaskazini ambao wanataka kupigana nchini Syria na pia kwa wale wanaojaribu kuondoka nchini humo. Inaaminika kuwa wawili miongoni mwa wahusika wa mashambulizi ya Ijumaa mjini Paris walipitia Uturuki, kwa mujibu wa viongozi.

Baadhi ya raia hao 8 wa Morocco tayari wamefukuzwa nchini Uturuki. Mahojiano ya wengine yanaendelea.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari vya Uturuki, kundi hilo lilikua linatazamia kwenda Ujerumani kwa kutumia barabara wakijifananisha kama wakimbizi. Maafisa wa Uturuki waliohojiwa wamesema hawaweza kuthibitisha habari hii.

Tayari mwezi huu, watu 41 kutoka Morocco, wanaotuhumiwa kutaka kujiunga na kundi la Islamic State (IS), walikamatwa katika Uwanja wa Ndege wa Ataturk.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.