Pata taarifa kuu
UN-BURUNDI-SIASA-USALAMA

Ufaransa yaiomba Jumuiya ya Kimataifa kukomesha machafuko Burundi

Katika mkutano wa Umoja wa Mataifa mjini New York kuhusu hali inayojiri Burndi Jumatatu Novemba 9, Ufaransa imeitaka jumuiya ya kimataifa kukomesha machafuko yanayoendelea katika taifa hilo dogo la Ukanda wa Maziwa makuu.

Naibu Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Alexis Lamek akitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa"kuchukua jukumu" kuhusu hali mbaya inayoendelea nchini Burundi.
Naibu Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Alexis Lamek akitoa wito kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa"kuchukua jukumu" kuhusu hali mbaya inayoendelea nchini Burundi. AFP PHOTO/Stan HONDA
Matangazo ya kibiashara

Ufaransa imechukua jitihada la azimio litakalojadiliwa wiki hii. Azimio hilo linalaani machafuko na wahusika wa machafuko hayo na linapendekeza vikwazo dhidi yao. Naibu Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Alexis Lamek amesema "anatiwa wasiwasi" na machafuko pamoja na hotuba zinazochochea chuki katika ukanda huu wa Afrika.

Ni wakati wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa "kuchukua jukumu lake", "vitendo vinapaswa kuanza kutekelezwa", Naibu Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, Alexis Lameki ametoa wito huo. " Tukumbuke kilichotokea katika nchi jirani ya Rwanda, miaka 21 iliyopita", alikumbusha mwenzake wa Uingereza. "Hatutokubali hali iliyotokea nchini Rwanda ijirudiye katika ukanda huo wa Maziwa Makuu", amesisitiza Mattyhew Rycroft, Balozi wa Uingereza katika Umoja wa Mataifa.

Azimio liliyowasilishwa na Ufaransa halitatua mgogoro nchini Burundi lakini kwa mujibu wa wanadiplomasia wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa, azimio hilo angalau linazishawishi pande husika kuketi kwenye meza ya mazungumzo. "Tulikuwa na hoja kwenda haraka, kwa sababu bado tunaweza kuzuia" licha ya hali tete inayoendelea kushuhudiwa nchini humo, wameeleza wanadiplomasia hao wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa.

Rasimu ya azimio inaamuru kumalizika kwa ghasia nchini Burundi, inalaani ukiukaji wa haki za binadamu, kauli zenye kuchochea chuki, mauaji yanayolenga baadhi ya watu na inatiwa wasiwasi kuhusu mvutano wa kisiasa ambao umesababisha karibu raia 200 000 kutoka Burundi kuikimbia nchi hiyo. Nakala hiyo inaomba viongozi wa Burundi kuwaadhibu wahusika na kuhakikisha ulinzi wa raia wake.

UN na ICC wametakiwa kufuatilia kwa karibu hali inayojiri Burundi

Azimio hilo lina Ibara mbili ambazo zitatakiwa kujadiiwa kwa kina. Ufaransa inajizuia uwezekano wa kuomba vikwazo dhidi ya wale waliohusika na ghasia. Lakini Urusi, China na wajumbe wa Afrika wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wanapinga mfumo huo wa vikwazo, amearifu mwandishi wetu mjini New York, Marie Bourreau.

Azimio pia linamuomba Ban Ki-moon kufikiria kuimarisha uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi na uwezekano wa kupeleka kikosiiwapo hali ya usalama itaendelea kuzorota. Urusi tayari imeonyesha wasiwasi wake wakati wa mazungumzo ya nje wa mkutano huo, ikiishtumu Ufaransa kutaka kuipindua serikali ya Burundi.

Aidha, Nakala hiyo inaitaka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) kufuatilia kwa karibu hali inayojiri nchini Burundi. Baraza la Usalama litajadili wiki hii rasimu ya azimio hilo. Kunahitajika idadi kubwa juu ya suala la vikwazo. Lakini suala la mauaji ya kimbari liligubika Jumatatu wiki hii mijadala ya Umoja wa Mataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.