Pata taarifa kuu
UN-DHO-UNICEF-VIFO kwa watoto

Vifo vya watoto wachanga vyagawanywa katika kipindi cha miaka 25 duniani

Vifo vya watoto wachanga duniani vimegawanywa mara mbili katika robo karne, lakini nchi 62 pekee kwa jumla ya nchi 195 zimefanikiwa kufikia malengo yaliyowekwa na Umoja wa Mataifa katika katika mukhtadha huu, kwa mujibu wa takwimu za Umoja wa Mataifa ziliyotolewa Jumatano wiki hii.

Chanjo ya mtoto, Agosti 20, 2015 Islamabad, nchini Pakistan.
Chanjo ya mtoto, Agosti 20, 2015 Islamabad, nchini Pakistan. AFP/AFP/Archives
Matangazo ya kibiashara

" Kiwango cha jumla cha vifo kwa watoto walio naumri wa miaka mitano kimepungua kwa 53% katika kipindi cha miaka 25 iliyopita" lakini nchi nyingi hazikufikia malengo yaliyowekwa katika mfumo wa malengo ya Milenia kwa Maendeleo (MDGs), kulingana na ripoti ya utafiti iliyochapishwa katika gazeti la matibabu la The Lancet.

Vifo vya watoto duniani vimepungua kutoka milioni 12.7 mwaka 1990 hadi milioni 5.9 mwaka 2015 (makadirio), kulingana na utafiti wa takwimu uliendeshwa na Umoja wa Mataifa na mashirika yake, ikiwa ni pamoja na Shirika la Afya Duniani (WHO ) na Unicef.

" Maendeleo endelevu yamepatikana kimataifa ili kuboresha maisha ya watoto kwa miaka hii 25 iliyopita ", wamebaini maafisa waliofanya kazi hii iliyoratibiwa na DanZhen You wa Unicef.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.