Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-MASHAMBULIZI-USALAMA

Nigeria: shambulio lawaua watu kadhaa Borno

Nchini Nigeria, mlipuko umetokea Jumanne wiki hii katika soko la kijiji cha Sabon Gari katika jimbo la Borno, Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Kwa mujibu wa tathmini ya awali, inakisiwa kuwa watu kadhaa wameuawa katika shambulio hilo.

Jimbo la Borno linakabiliwa mara kwa mara na mashamblizi. Hapa, ni baada ya mlipuko katika soko katika jimbo la Maiduguri, Julai 31 mwaka 2015.
Jimbo la Borno linakabiliwa mara kwa mara na mashamblizi. Hapa, ni baada ya mlipuko katika soko katika jimbo la Maiduguri, Julai 31 mwaka 2015. AFP PHOTO
Matangazo ya kibiashara

Mlipuko huo umetokea alaasiri katika soko la kila wiki la Sabon Gari, katika kijiji kilio kusini mwa Maiduguri. Baada ya mlipuko huo, kila moja alikimbia kutoka eneo hilo kwa kuhofia kutokea milipuko mingine.

Chanzo cha polisi kimeilezea RFI kwamba soko hilo limefungwa na vikosi vya usalama vimewekwa eneo hilo ili kubaini mazingira kamili ya mlipuko huo. Milpuko huo umetokea kwenye eneo kunakouzwa simu, katikati ya soko. Taarifa hii imethibitishwa na mmoja wa wajumbe wa kundi linalojihami. Kundi hili liliundwa kwa minajili ya kupambana dhidi ya Boko Haram kwa ushirikiano na vikosi vya jeshi. Kwa mujibu wa raia huyo, bomu lilikua lilifichwa katika mfuko unaotumiwa kwa kufukuza wadudu. Bomu hilo liliingizwa katika soko, kisha ukaachwa humo kabla ya kulipuka

Muuguzi wa hospitali kuu ya Biu, iliyoko kilomita 50 kutoka soko hio, ameliambia shirika la habari la Ufaransa (AFP) kwamba alipokea maiti 47 na majeruhi 50, ambao walijeruhiwa vikali. Hakuna kundi hata moja ambalo limekiri kuhusika na shambulio hilo. Lakini kwa mujibu wa mashahidi walionukuliwa na AFP, kundi la Boko Haram linasadikiwa kutekeleza shambulio hilo. Jimbo la Borno linachukuliwa kuwa kitovu cha waasi wa Kiislam. Mwezi Julai, mwanamke mmoja aliyejitoa mhanga aliwaua watu wanne katik aeneo linalodhibitiwa na jeshi katika mji wa Sabon Gari.

Jimbo la Borno lalengwa

Jimbo la Borno limekua likilengwa na mashambulizi ya kundi la Islamic State Afrika Magharibi. Borno ni ngome kuu ya Abubakar Shekau, kiongozi wa kundi hilo la kijeshi, na wapiganaji wake. Kuna watu ambao anashirikiana naye katika jimbo hilo. Na watu hao wanatambua vizuri eneo lilio karibu ya ziwa Chad. Hata hivyo, kwa miezi kadhaa, vikosi vya jeshi na polisi nchini Nigeria wamezidisha ulinzi katika maeneo mbalimbali, huku wakishirikiana na watu waliojitilea kwa kuimarisa usalama katika maeneo yao. Lakini vikosi hivyo vimekua vikikabiliana na wapiganaji wa kundi la Islamic State Afrika Magharibi (Boko Haram).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.