Pata taarifa kuu
TUNISIA-UGAIDI-USALAMA

Tunisia: rais Beji Caïd Essebsi atangaza hali ya hatari

Serikali ya Tunisia imetangaza Jumamosi Julai 4 hali ya hatari kwa muda wa siku thelathini, mbadala. Uamuzi huu wa Beji Caid Essebsi unavipa uwezo wa dharura vikosi vya usalama na ulinzi. Rais amefafanua uamzi wake huo katika hotuba yake kwa taifa.

Askari polisi wakipiga karibuhoteli Imperial Marhaba katika mji wa Sousse, uliyoshambuliwa Juni 26.
Askari polisi wakipiga karibuhoteli Imperial Marhaba katika mji wa Sousse, uliyoshambuliwa Juni 26. REUTERS/Zohra Bensemra
Matangazo ya kibiashara

" Tuko katika hali ya vita. Mazingira ya kipekee huhalalisha hatua ya kipekee “, amesema Beji Caïd Essebsi.

Katika hotuba yake kwa taifa, hotuba ambayo ilidumu dakika ishirini, rais wa Tunisia amekubali kuwa nchi yake haikuwa na utamaduni wa kupambana dhidi ya ugaidi na imekua haina rasilimali watu na vifaa ili kukabiliana na janga hilo. ECB pia ameelezea tishio linaloendelea kuikabili nchi ya Libya, ambapo wanajihadi wamekua wakipewa mafunzo kabla ya kuvuka mipaka na kufanya uhalifu wao nchini Tunisia.

Hali ya hatari imetangazwa nchi nzima kwa muda wa siku thelathini, mbadala. Hatua hii hasa inaimarisha uwezo wa jeshi na vikosi vya usalama. Hatua hii inawapa viongozi uwezo wa kuzuia uhuru kwa mashirika ya kiraia, ikiwa ni pamoja na haki ya kufanya mikutano na migomo. Hatua hi pia inaweza kwenda sambamba na udhibiti wa vyombo vya habari.

Tangazo hili la hali ya hatari limetokea masaa 24 baada ya Waziri mkuu Habib Essid, ambaye katika mahojiano na BBC, alikiri kwamba polisi ilichelewa mno kuingilia kati na kusimamisha mauaji ya Juni 26 katika mji wa kitalii wa Sousse. Vyombo vya habari vya Uingereza vimekosoa vikali mwenendo wa vikosi vya usalama vya Tunisia dhidi ya shambulio hilo lililogharimu maisha ya watu 38, ikiwa ni pamoja na raia 30 wa Uingereza.

Mji wa Sousse uliwahi kulengwa na mashambulizi ya kujitoa mhanga mwezi Oktoba mwaka 2013. Ingawa shambulio hilo lilifeli, laikini polisi haikua makini na kuweza kutoa ulinzi wa kutosha katika mji huo unaotembelewa na watu wengi kutoka mataifa mbalimbali duniani.

Kufuatia shambulio hilo, viongozi kadhaa wa kisiasa nchini Tunisia, ikiwa ni pamoja na gavana wa Sousse, walifukuzwa kazi, alitangaza Jumamosi mshauri wa Waziri mkuu. Wakurugenzi wa tatu wa usalama walinga'tuliwa kwenye nyadhifa zao mapema wiki.

Tahadhari na uaminifu

Miongoni mwa waangalizi wa masuala ya kijeshi, Moctar Ben Nasser, afisa mstaafu, amekumbusha kuwa kipindi cha nyuma cha hali ya hatari iliyotangazwa baada ya kuangushwa utawala wa Ben Ali mwezi Machi mwaka 2014, hali hiyo haikuzaa matunda yoyote na haikuzuia magaidi kuendelea kujidhatiti nchini Tunisia. Pia amezungumzia gharama kubwa ya fedha za ziada zilizotolewa kwa wanajeshi, wakati ambapo nchi ya Tunisia iko katika mstairi mwekundu.

Kiongozi wa shirika la Haki za Binadamu nchini Tunisia , kwa upande wake, ana wasiwasi kwamba hali ya hatari imekuja kukiuka haki za msingi. Kwa upande wake, hatua hiyo ni muhimu, lakini haipaswi kuchukua muda mrefu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.