Pata taarifa kuu
MOROCCO-UHAMIAJI-USALAMA

Morocco: mamia ya wahamiaji wakimbilia katika Kanisa la Tanger

Nchini Morocco, mamia ya wahamiaji kutoka kusini mwa jangwa la Sahara wamekimbilia katika vitongoji vya mji wa Tanger na wengine wameomba hifadhi katika Kanisa la mji huo.

Wahamiaji kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara wakimbia operesheni ya polisi Julai 2 mwaka 2015,  mjini Tanger, Morocco.
Wahamiaji kutoka kusini mwa Jangwa la Sahara wakimbia operesheni ya polisi Julai 2 mwaka 2015, mjini Tanger, Morocco. AFP PHOTO / FADEL SENNA
Matangazo ya kibiashara

Wahamiaji hao walikimbia operesheni ya polisi ambayo mwanzoni mwa wiki hii iliyafunga majengo kadhaa yaliyokua yakikaliwa kinyume cha sheria katika mtaa mmoja wa mji wa Tanger.

Hata hivyo misaada imekua ikitolewa katika Kanisa hilo ili kuwasaidia wahamiaji ambao wengi wao ni wanawake na watoto.

Kwa siku kadhaa, wakimbizi wamekusanyika katika Kanisa la watu kutoka Uhispania mjini Tanger. Lakini kwa sasa, wanawake na watoto wanalala ndani ya Kanisa hilok, huku wanawake na watoto wakilazimika kulala nje usiku. Hali ya usafi ni duni kwa sababu kuna choo moja tu ya kuogea kwa jumla ya watu 600 wanaoomba hifadhi eneo hilo.

Tatizo la kuoga, ukosefu wa maji, ukosefu wa chakula, Kanisa haina uwezo wa kukidhi mahitaji ya wakimbizi wote hao. Kwa sasa raia wameanza kuwatolea wahamiaji hao msaada wa chakula na vifaa vingine kama alivyoiambia RFI mwanamke kutoka Guinea ambaye amekua akijaribu kuwafariji wahamiaji hao.

" Mimi sina bajeti au fedha. Najaribu kusaidia kimaadili tu, au kwa chakula, najaribu pia kujadili mabweni kwa ajili ya watu hao ", amesema mwanamke huyo kutoka Guinea. "Siwezi kuona ndugu zangu wahamiaji wakilala nje ambapo wanaweza kuliwa na wanyama ", ameendelea kusema mwana mke huyo.

Kama baadhi wameondolea na polisi katika majengo walipokua wakiishi, wakimbizi wengine walinyanyaswa siku za hivi karibuni na majirani zao kutokana na ubaguzi wa rangi aidha wakaazi wengine wa mji wa Tanger ambao walipata nafasi ya kuwachukia zaidi wahamiaji hao kufuatia operesheni iliyoendeshwa na polisi dhidi yao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.