Pata taarifa kuu
AU-JOHANNESBURG-MKUTANO-USALAMA-SIASA

Hali ya Burundi katika ajenda ya mazungumzo ya mkutano wa AU

Mkutano wa kilele wa 25 wa Umoja wa Afrika unazunduliwa Alhamisi wiki hii nchini Afrika Kusini. Mkutano huo ni wa ngazi ya mawaziri wa mambo ya nje kutoka nchi za bara la Afrika, na utafuatiwa na mkutano wa marais ambao umepangwa kufanyika mwishoni mwa juma hili.

Nkosazana Dlamini Zuma, Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika.
Nkosazana Dlamini Zuma, Rais wa Tume ya Umoja wa Afrika. AFP/ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Kauli mbiyu ya mkutano huo ni “ Mwaka wa uwezeshaji wa wanawake”, lakini migogoro mbalimbali inayoshuhudiwa barani Afrika itatawala katika ajenda ya mkutano huo. Migogoro hiyo ni pamoja na vita dhidi ya ugaidi, hali inayojiri Libya, Sudan Kusini hasa Burundi.

Inawezekana kuwa rais wa Burundi Pierre Nkurunziza asishiriki mkutano huo wa Umoja wa Afrika utakaofanyika katika mji wa Johannesburg, Afrika Kusini. Mara ya mwisho Pierre Nkurunziza aliondoka Burundi na kujielekeza Dar es Salaam, Tanzania, kushiriki mkutano wa marais wa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki kuhusu mgogoro wa Burundi, ambapo kundi la maafisa wa jeshi walijaribu kuupinduwa utawala wake bila mafanikio.

Mkutano huo utajikita hasa na mgogoro wa Burundi na majaribio ya baadhi ya marais ya kuwania awamu ya tatu. Hii imekua ni kasumba kwa marais wa Afrika kubadili Katiba za nchi zao ili waendelee kusalia madarakani.

Umoja wa Afrika ulionesha msimamo wake kuhusu muhula wa tatu wa rais Pierre Nkurunziza. Rais wa Kamati ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma alipinga rais wa Burundi kuwania muhula watatu, akibaini kwamba rais Nkurunziza anatakiwa kuheshimu Katiba ya nchi na mkataba wa amani na maridhiano wa Arusha.

Kwa upande wake Taasisi ya Mafunzo ya Usalama imebaini kwamba hata kama ujumbe wa Umoja wa Afrika uko wazi, hauendani na vitendo.

Umoja wa Afrika una sheria zake, kama vile Mkataba wa Afrika kuhusu Demokrasia, Uchaguzi na Utawala, ambao unazichukulia vikwazo nchi ambazo haziheshimu kanuni fulani, lakini Umoja wa Afrika hautumii sheria hizo.

Kuna uwezekano mdogo kwamba Umoja wa Afrika unaweza kutoa msimamo mkali dhidi ya rais wa Burundi. Hasa kwa vile rais wa Umoja wa Afrika si mwingine zaidi ya Robert Mugabe, ambaye ni rais wa Zimbabwe kwa muhula wa sita sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.