Pata taarifa kuu
AFRIKA-BIASHARA HURIA-UCHUMI

Makubaliano ya biashara huria kati ya nchi 26 za Afrika Mashariki

Nchi 26 za Afrika Mashariki zimetia saini kwenye mkataba wa biashara huria leo Jumatano mjini Sharm el-Sheikh, nchini Misri. Viongozi waandamizi wanakutana tangu mwanzoni mwa wiki hii katika mji huo ili kukamilisha nakala inayounda eneo hilo linalojumuisha nusu ya nchi za Mashariki ya bara la Afrika.

Katibu Mkuu wa COMESA, Sindiso Ngwenya (katikati amesimama), akiwasilisha hati ya mkataba wa biashara huria kwa mawaziri na wawakilishi wa nchi 26 za Afrika Mashariki, Juni 8 mwaka 2015. COMESA
Katibu Mkuu wa COMESA, Sindiso Ngwenya (katikati amesimama), akiwasilisha hati ya mkataba wa biashara huria kwa mawaziri na wawakilishi wa nchi 26 za Afrika Mashariki, Juni 8 mwaka 2015. COMESA COMESA
Matangazo ya kibiashara

Hii ni hatua moja zaidi katika safari ndefu kuelekea katika ushirikiano wa kiuchumi wa nchi hamsini katika maendeleo tofauti.

Ingelichukua miaka mitano ya mazungumzo ili kufikia kuundwa kwa " ushirikiano huo wa pande tatu ", katika eneo hilo la biashara huria linaloanzia toka Cape Town nchini Afrika Kusini hadi Cairo, Misri. Hali hii imetokana na uimarishaji wa Kanda tatu za kiuchumi, ambapo hakuna Ukanda hata mmoja ambao umekamilisha ushirikiano wake ikiwa ni pamoja na Soko la Pamoja la Nchi za Kusini mwa Afrika na Mashariki (COMESA), Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) na Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC).

Nchi 26 kutoka " majimbo mtatu " zina wakaazi milioni 625 na zina pato la taifa la pamoja la Euro bilioni 900. Mkataba wa biashara huria unatazamia kuunda bei ya pamoja ya ushuru na kuondoa vikwazo visivyokuwa vya ushuru. Kila nchi imekua ikilinda bidhaa zake na hii ikiwa ndio moja ya vikwazo vya mzunguko wa bidhaa kutoka nchi moja kuingi nch nyingine.

Nakala hii inapaswa kuunganisha sera za biashara. Hatimaye, watiaji saini wa mkataba huu ni wanatarajia kupanda kwa asilimia 20 hadi 30 ya biashara kati ya nchi wanachama wa eneo hili.

Mafanikio ya wazo la biashara huria pia inategemea ile ya NEPAD. Ushirikiano mpya wa Maendeleo ya Afrika, ambayo inatoa hasa kuboresha miudombinu hususan ujenzi wa barabara, reli na njia nyingine za mawasiliano ili kukuza bara biashara katika bara la Afrika. Baada ya kusainiwa kwa mkataba wa Sharm el-Sheikh, nchi 26 wanachama wa eneo jipya la biashara huria watakuwa na mwaka mmoja wa kuridhia mkataba huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.