Pata taarifa kuu
WHO-LIBERIA-AFYA

WHO : Liberia haina tena Ebola

Shirika la Afya duniani WHO, limetangaza rasmi Jumamosi mwishoni mwa juma hili kwamba Liberia haina tena ugonjwa wa Ebola. Mtu wa mwisho alifariki baada ya kuambukizwa virusi vya Ebola siku 42 ziliyopita.

Kiijana huyo kutoka Liberia akipewa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola katika hospitali ya Redemption ya mji wa Monrovia.
Kiijana huyo kutoka Liberia akipewa chanjo dhidi ya virusi vya Ebola katika hospitali ya Redemption ya mji wa Monrovia. RFI/Sébastien Nemeth
Matangazo ya kibiashara

Liberia ni moja ya nchi za Afrika magharibi iliyoathiriwa zaidi na ugonjwa wa Ebola. Kwa sasa nchi hiyo inaonekana kujikwamua na kujiendeleza baada ya kukabiliana na ugonjwa huo hatari kwa binadamu.

Zaidi ya watu 10,000 waliambukizwa virusi vya Ebola, huku watu 4,573 wakifariki baada ya kuambukizwa virusi vya ugonjwa huo.

Shirika la Afya Duniani WHO, limekaribisha juhudi zilizofanywa na Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, ambaye kwa mujibu wa WHO, alihamasisha raia wake na kubaini tangu mwanzo kuwa Ebola ni tishio kwa nchi ya Liberia. WHO inachukulia kwa kile inachosema kuwa hakuna maambukizi ya virusi vya Ebola ambavyo vimeripotiwa ndani ya siku 42, na hivyo kusema kuwa Liberia haina tena ugonjwa wa Ebola.

“ Kufuatia kipindi hiki cha siku 42, kumekua na umakini katika hali ya kuchunguza kesi ya maambukizi ya virusi vya Ebola, na hapakuwepo na maambukizi yoyote tangu kuanza kipindi hicho. Tuna uhakika kwamba ugonjwa wa Ebola umetokomezwa ", Dk Bruce Aylward, mkurugenzi mkuu msaidizi wa WHO ameithibitishia RFI mjini Geneva, Uswisi.

WHO imekaribisha kazi ya ya uhamasishaji iliyotekelezwa na wanajamii, ikiwa ni pamoja na viongozi wa vijiji, taasisi za wanawake na vijana au makundi ya kidini. Ujumbe wa watu hao umepelekea kutokomezwa kwa ugonjwa wa Ebola.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.