Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-HRW-UNICEF-UTEKAJI NYARA-SIASA

Askari watoto Sudan Kusini: HRW yakosoa msimamo wa serikali

Taarifa ya kutekwa nyara kwa watoto 89 walio na umri kati ya 13 na 18 nchini Sudani Kusini imekua ni kero kwa shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Right Watch.

Askari watoto wakati wa sherehe za kupokonywa silaha, kurejeshwa katika maisha ya kiraia na kuwaunganisha na jamii zao. Sherehe ambazo zilisimamiwa na UNICEF, Februari 10 mwaka 2015, katika jimbo la Jonglei, Sudani Kusini.
Askari watoto wakati wa sherehe za kupokonywa silaha, kurejeshwa katika maisha ya kiraia na kuwaunganisha na jamii zao. Sherehe ambazo zilisimamiwa na UNICEF, Februari 10 mwaka 2015, katika jimbo la Jonglei, Sudani Kusini. AFP PHOTO/Charles LOMODONG
Matangazo ya kibiashara

Kitendo hiki cha kuwateka nyara watoto hawa kiliendesha kaskazini mwa nchi, katika mji wa Wau Shilluk, ambapo raia 100,000 waliomba hifadhi miezi ya hivi karibuni katika mji huo.

Kwa mujibu wa Human Right Watch, hali hiyo inatokea wakati ambapo mji huo unakabiliwa na changamoto nyingi, huku ukiwa mikononi mwa jeshi la serikali.

Skye Wheeler, ambaye ni mtafiti katika shirika hilo, ameelezea kukerwa na kitendo hicho, kwani Human Right Watch iliomba serikali ya Sudani Kusini hivi karibuni kukabiliana na zoezi la kusajili watoto katika jeshi.

“ Jambo ambalo halieleweki, ni kuona watoto wote hawa wametekwa kwa wakati mmoja, na hii inamaanisha kuwa vitendo hivi vimekithiri kutokana na msimamo wa serikali wa kutowaadhibu watu wanohusika na kusajili watoto katika jeshi au makundi ya waasi”, amesema mtafiti huyo wa Human Right Watch.

Skye Wheeler, ameongeza kuwa ni kwa kipindi cha miaka zaidi ya kumi na mbili sasa hali hii ikiendelea kushuhusiwa Sudani Kusini.

“ Serikali ya Sudani Kusini ilikua imejitahidi kupatia suluhu suala hili, baada ya kutia saini na serikali ya Khartoum kwenye mkataba wa amani kwa kuwarejesha katika maisha ya kiraia watoto waliokua wakitumiwa katika jeshi. Lakini vitendo hvi vya kuwasajili watoto katika jeshi au makundi ya waasi yalirudi kushuhuiwa tangu kuzuka kwa machafuko mapya mwezi Desemba mwaka 2013”, amesema Skye Wheeler,.

Jumamosi, juma hili lililopita, Unicef ililani kitendo hiki cha kuwateka nyara watoto 89. Kitendo ambacho kilitekelezwa na kundi la watu wenye silaha ambao hawajafahamika.

Watoto 12,000 ndio wamesajiliwa katika jeshi na makundi ya waasi tangu Desemba mwaka 2013 nchini Sudani Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.