Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-UCHAGUZI-Usalama-SIASA

Nigeria yasogeza mbele uchaguzi wa rais kutokana na sababu za kiusalama

Nchi ya Nigeria imeahirisha uchaguzi wa rais uliopangwa kufanyika Jumamosi ijayo kutokana na sababu za kiusalama kufuatia kukuongezeka kwa mgogoro wa Boko Haram.    

Rais wa Nigéria, Goodluck Jonathan
Rais wa Nigéria, Goodluck Jonathan REUTERS/Afolabi Sotunde
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii inakipa nafasi muhimu chama tawala wakati huu kinapokabiliana na changamoto ngumu kutoka vyama vya upinzani.

Tangazo la kucheleweshwa kwa uchaguzi huo kwa majuma sita limetolewa baada ya wakuu wa usalama kusema kuwa jeshi linahitaji muda zaidi wa kurejesha maeneo yaliyo chini ya udhibiti wa Boko Haram,wanamgambo wenye msimamo mkali wa Kiislam ambao wameteka eneo kubwa kaskazini mashariki mwa Nigeria.

Akitangaza kuhusu mabadiliko hayo ya ratiba ya uchaguzi mwenyekiti wa Tume huru ya uchaguzi nchini Nigeria Attahiru Jega amesema uchaguzi wa rais na wabunge utafanyika tarehe 28 Machi badala ya Februari 14 kama ilivyopangwa awali .

Uchaguzi wa magavana na bunge la kitaifa utafanyika tarehe 11 mwezi Aprili, ameongeza Jega.

Jega amesema wakuu wa usalama wameshauri kwamba uchaguzi lazima uahirishwe kwa muda wa wiki sita kwa kuwa operesheni za kijeshi kaskazini mashariki mwa nchi hiyo zimesababisha ukosefu wa askari wa kulinda usalama wakati wa uchaguzi.

Aidha amewaambia waandishi wa habari kuwa kama usalama wa wafanyakazi, wapiga kura, waangalizi wa uchaguzi na vifaa vya uchaguzi haviwezi kupata uhakika wa usalama, maisha ya vijana wasio na hatia na wanawake na matarajio ya uchaguzi huru, wa haki na wa kuaminika yatakuwa hatarini sana.

Rais Goodluck Jonathan amefungwa katika mapambano makali na mgombea wa chama kikuu cha upinzani ,kiongozi wa zamani wa jeshi Muhammadu Buhari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.