Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-AFYA-MAZUNGUMZO-Usalama-Jamii

Salva Kiir augua ghafla

Rais wa Soudan Kusini, Salva Kirr, amelazwa hospitali baada ya kuugua ghafla, na kukimbizwa katika hospitali ya mjini Addis Ababa, Ethiopia.

Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir, amelazwa hospitali, Addis Ababa, Ethiopia.
Rais wa Sudani Kusini, Salva Kiir, amelazwa hospitali, Addis Ababa, Ethiopia. Reuters/Goran Tomasevic
Matangazo ya kibiashara

Hayo yanatokea baada ya rais Kiir kuanzisha mazungumzo Jumatano wiki hii na kiongozi wa waasi Riek Machar kujadili masuala kwa lengo la kukomesha vita viliyosababisha maafa makubwa ambavyo vimedumu kwa zaidi ya mwaka mmoja nchini Sudan Kusini.

Pande hizi mbili bado hazijaafikiana kuhusu kuundwa kwa serikali ya mpito.

Maelfu ya watu wamekufa na zaidi ya milioni wameyakimbia makazi yao tangu kuanza kwa vita vya wenyewe kwa wenyewe mwezi Desemba mwaka 2013.

Mashahidi wamesema kwamba rais Kiir, alianza kuvuja damu kutoka puani.
Kabla ya kuugua, hapo jana Jumatano Kiir alifanya mazungumzo na kiongozi wa waasi Riek Machar ambapo alimtaka kupuuzilia mbali maswala yanayochochea machafuko ili kumaliza Machafuko hayo ambayo yamedumu zaidi ya mwaka mmoja sasa.

Viongozi wa kikanda, wanakutana baadaye leo, kushinikiza pande zote kufikia makubaliano ili kumaliza vita.

Hata hivyo rais wa Mali, Ibrahim Boubacar Keita, kwa mujibu wa shirika la habari la Ufaransa (AFP) huenda amefuta ziara yake nchini Ethiopia kushiriki katika mkutano wa kilele wa marais na viongozi wa Afrika, na amejielekeza katika mji wa Gao, ambapo maandamano na vurugu dhidi ya vikosi vya Umoja wa Mataifa Minusma yaliyosababisha vifo vya watu wengi.

Hii ni mara ya kwanza rais huyo kujielekeza kaskazini mwa Mali tangu achaguliwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.