Pata taarifa kuu
MADAGASCAR-Siasa-Maridhiano

Waziri mkuu mpya Madagascar

Siku mbili baada ya kujiuzulu kwa Roger Kolo, rais wa Madagascar amemteua Jean Ravelonarivo kuwa Waziri mkuu wa nchi hiyo.

Kolo Roger (pichani) alijiuzulu serikalini mnamo Januari 12 mwaka 2015.
Kolo Roger (pichani) alijiuzulu serikalini mnamo Januari 12 mwaka 2015. AFP PHOTO / RIJASOLO
Matangazo ya kibiashara

Ravelonarivo haijulikani na raia wengi nchini Madagascar, hadi sasa alikua bado mkuu wa kikiosi cha wanajeshi wa anga.

Ravelonarivo alikuwa ni kwenye orodha ya wagombea kumi waliopendekezwa Jumanne Januari 13 kwa rais na kundi la Wabunge kutoka vyama vinavyounga mkono serikali.

Tangazo hilo lilitolewa jioni Jumatano wiki hii katika Ikulu ya rais. Katibu Mkuu wa kwenye Ikulu, Roger Ralala ndiye aliyesoma sheria ya kirais inayomteua Jean Ravelonarivo kuwa Waziri mkuu wa Madagascar.

" Sheria ya kirais 2015-2021 imemteua Waziri mkuu, mkuu wa kikosi cha wanajeshi wa anga Jean Ravelonarivo",amesema Roger Ralala. Wajumbe wa serikali madarakani wataendelea kushikilia nyadhifa zao hadi litakapoteuliwa baraza jipya la mawaziri, ameendelea kusema Ralala.

Licha ya kuwa Jean Ravelonarivo, ambaye bado anahudumu katika jeshi, ni mshirika wa karibu wa rais Herry Rajaonarimampianina, hajulikani katika ulimwengu wa kisiasa.

Hata hivyo, Waziri mkuu huyo mpya haungwi mkono na Wabunge wa upinzani, kwani saa chache kabla ya uteuzi wake, muungano wa wabunge kutoka upinzani ulidai haki ya kupendekeza mgombea wao.

Kwa mujibu wa Ibara ya 54 ya Katiba, rais lanatakiwa kuchagua Waziri mkuu wake kutoka kwenye orodha ya watu waliopendekezwa na kundi wengi katika Bunge kutoka vyama vinavyomuunga mkono.

Maridhiano ya kitaifa

Aidha, mkutano wa maridhiano ya kitaifa unaendelea leo Alhamisi nchini Madagascar. Rais na watangulizi wake wanne wanakutana tena hadi leo jioni katika mji wa Ivato.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.