Pata taarifa kuu
DRC-PPRD-UDPS-KATUMBI-SIASA

Moise Katumbi apokelewa kwa vifijo

Mkuu wa mkoa wa Katanga Moise Katumbi Chapwe amerejea nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumanne Desemba 23 mwaka 2014. Kurejea kwake kulikua kukisubiriwa na maelfu ya raia wakazi wa mkoa wa Katanga.

Mkuu wa mkoa wa Katanga, Moise Katumbi, akiwa pia mmiliki wa klabu ya Soka ya Tout Puissan Mazembe.
Mkuu wa mkoa wa Katanga, Moise Katumbi, akiwa pia mmiliki wa klabu ya Soka ya Tout Puissan Mazembe. AFP PHOTO / ISSOUF SANOGO
Matangazo ya kibiashara

Alipowasili katika uwanja wa ndege Jumanne Desemba 23 katika mji wa Lubumbashi, Moise katumbi alipokelewa na mamia kwa maelfu ya raia wakiwemo wafuasi wa chama chake cha PPRD. Kukosekana kwake kwa kipindi cha miezi miwili kulizua habari za kutatanisha.

Mkuu huyo wa mkoa wa Katanga anashukiwa kwamba anataka kugombea dhidi ya rais wa sasa wa Congo Joseph Kabila au kujiondoa katika chama tawala cha PPRD.

Moise katumbi, amepokelewa na makundi mbali mbali ya wanasiasa, ikiwa ni pamoja na wafuasi wa chama tawala na vyama kinavyoshirikiana navyo, upinzani na wawakilishi wa mashirika ya kiraia.

“ Hatumuudhi mtu yoyote, Mungu ndiye muumba. Tunawaombea hata maadui zetu. Tuwaombee hata wale wasio tupenda. Tuwaombee ili Mungu atubariki”, amesema Moise katumbi Chapwe.

Wakati huo huo chama cha upinzani cha UDPS cha Etienne Tshisekedi wa Mulumba kimetolea wito wa kufanyika kwa mazungumzo yatakayosimamiwa na jumuiya ya kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.