Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-ZANU-PF-SIASA

Zimbabwe: Mugabe ajipa madaraka zaidi

Rais wa zimbabwe Robert Mugabe ameendelea kushikilia chama tawala cha Zanu-PF kama chama chake biinafsi.

Robert Mugabe, katika mkutano wa 34 wa SADC, zambia, Agosti 18 mwaka 2014.
Robert Mugabe, katika mkutano wa 34 wa SADC, zambia, Agosti 18 mwaka 2014. REUTERS/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Ikisalia wiki moja ili mkutano mkuu wa chama hicho ufanyike, ambapo anatazamiwa kuongezwa muhula kwa kuendelea kushikilia nafasi hiyo kwenye chama, Robert Mugabe amejipa madaraka yote katika chama, ikiwa ni pamoja na kumlazimisha mrithi wake katika uongozi wa nchi.

Makamu wa rais wa Zimbabwe Joice Mujuru ameondolewa katika Kamati kuu ya chama tawala Zanu-PF kwa tuhma za kupanga mbinu za kumuua rais Robert Mugabe na pia anatuhumiwa kuhusika na wizi wa fedha kutoka Kampuni za serikali.

Bi Mujuru amekuwa akishtumiwa na Mke wa Mugabe, Grace Mugabe wakati huu siasa zikiendelea ndani ya chama cha Zanu-PF kuhusu ni nani atakayemrithi Mugabe mwenye umri wa miaka 90.

Kuondolewa kwa Mujuru katika Kamati ya Zanu-PF kunakuja siku chache kabla ya kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa chama hicho tarehe 3 mwezi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.