Pata taarifa kuu
MISRI-UFARANSA-Diplomasia

Al-Sissi ziarani Paris: Ufaransa yajaribu kufufua ushirikiano na Misri

Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sissi anatazamiwa kukutana Jumatano Novemba 26 na rais wa Ufaransa Francois Hollande na maofisa kadhaa wa serikali ya ufaransa, ikiwa ni pamoja Waziri wa mambo ya nje Laurent Fabius, kabla ya chakula cha jioni na Waziri wa Ulinzi Jean-Yves Le Drian ambapo suala la ushirikiano wa kijeshi litajadiliwa.

Abdel Fattah Al-Sissi anatazamiwa kukutana Novemba 26 na rais wa Ufaransa, François Hollande na maofisa wa serikali ya Ufaransa.
Abdel Fattah Al-Sissi anatazamiwa kukutana Novemba 26 na rais wa Ufaransa, François Hollande na maofisa wa serikali ya Ufaransa. REUTERS/The Egyptian Presidency/Handout
Matangazo ya kibiashara

Baada ya miaka thelathini ya uhusiano karibu wa kipekee kati ya Marekani na Misri, Paris inatarajia kufufua uhusiano na Cairo pamoja na kushiriki katika zoezi la kuimarisha jeshi katika ulimwengu wa kisasa.

Mashambulizi ya makundi ya wapiganaji wa kijihadi dhidi ya kituo cha ukaguzi katika jimbo la Farafra, karibu na mpaka wa Libya ulisababisha madhara makubwa kwa jeshi la Misri. Maafisa ishirini na mbili walinzi wa mpaka waliuawa tarehe 19 mwezi Julai.

Hivi karibuni, operesheni iliyoendeshwa dhidi ya jeshi la misri liliyokua likipiga doria katika bahari ya Mediterania na kusababisha kutoweka kwa wanajeshi wanane ilionesha kuwa Misri inakabiliwa na tishio la kigaidi . " Rais Sissi anatakiwa kwenda haraka ili kuimarisha usalama nchini mwake, lakini pia kuweka sawa uchumi wa chi yake", watu walio karibu na waziri wa ulinzi wa Ufaransa wameonya.

"Misri imekua ikijaribu kushirikana na nchi mbalimbali kwa minajijili ya kutafuta nchi ambazo zitakua zikiiuzia silaha. "Urusi imeanza biashara hiyo", viongozi nchini Ufaransa wamebaini.

Lakini Ufaransa ilishindia mapema mwaka huu mkataba wa mauzo ya manuari nne kwa jeshi la majini la Misri, ambapo tatu kati ya manuari hizo nne zitatengezewa mjini Alexandria nchini Misri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.