Pata taarifa kuu
BURUNDI-UPINZANI-CENI-UTAWALA-SIASA-USALAMA

Burundi: zoezi la kuandika wapiga kura laanza

Zoezi la kujiorodhesha kwenye daftari la wapiga kura limeanza leo Jumatatu Novemba 24 nchini Burundi, licha ya kuendelea kwa mvutano kati ya vyama vya siasa na tume huru ya uchaguzi (Ceni).

Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Burundi, Pierre-Claver Ndayicariye.
Mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi nchini Burundi, Pierre-Claver Ndayicariye. DR
Matangazo ya kibiashara

Zaidi ya raia milioni 4 ambao wametimiza umri wa miaka wanatazamiwa kuanza kujiandikisha tangu leo Jumatatu Novemba 24 kwenye daftari la wapigakura. Zoezi hilo linaanza wakati ambapo hali ya mvutano kati ya vyama vya siasa na tume huru ya uchaguzi  (Ceni) ikiendelea.

Vyama vya siasa hususan vyama vya upinzani vimekua vikinyooshea kidole cha lawama tume huru ya uchaguzi kwamba imekua  ikiendesha shughuli zake kwa ushawishi wa chama tawala cha Cndd-Fdd.

Upinzani umesema utaratibu huo unaotumiwa na tume huru ya uchaguzi unaonesha kwamba uchaguzi mkuu utakaofanyika hapo mwakani utagubikwa na kasoro nyingi. Upinzani nchini Burundi umesema hauna imani na tume huru ya uchaguzi (Ceni).

Jumamosi Novemba 22, vyama 10 vya upinzani viliiandikia tume huru ya uchaguzi vikiiomba iahirisha zoezi la uandikishaji hadi mwezi Desemba, vikibaini kwamba zoezi hilo limeitishwa haraka bila hata hivo kuepo na maelewano kati ya vyama vya siasa na tume huru ya uchaguzi.

Baadhi ya vyama vya upinzani vimewataka wafuasi wao kutoitikia zoezi hilo.

Tume huru ya uchaguzi (Ceni) kupitia msemaji wake, Prosper Ntahogwamiye, imesema zoezi hilo linapaswa kuanza leo Jumatatu Novemba 24. Ceni imekua ikivituhumu vyama vya upinzani kwamba vinalenga kuzorotesha shughuli zake.

Vyama vya upinzani vilimpinga mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Pierre-Claver Ndayicariye na msemaji wa tume hiyo, mara tu baada majina yao kupitishwa na Bunge mezi minane iliyopita.

Itafahamika kwamba  wabunge kutoka vyama vya Uprona na Frodebu Nyakuri walijiodoa katika kikao hicho cha Bunge kiliyopitisha majina hayo. Pierre-Claver Ndayicariye na Prosper Ntahogwamiye walishikilia nafasi hizo kwenye tume huru ya uchaguzi iliyoandaa uchaguzi wa mwaka 2010, ambapo vyama vya upinzani vilijiondoa mapema katika uchaguzi wa mwanzo wa madiwani vikibaini kwamba uligubikwa na wizi.

Mara kadhaa upinzani uliomba mwenyekiti wa tume huru ya uchaguzi Pierre-Claver Ndayicariye na msemaji wa Ceni, Prosper Ntahogwamiye wajiuzulu, vikibaini kwamba havina imani na watu hao.

Kwa upande wake kiongozi wa chama tawala Cndd-fdd, Pascal Nyabenda, ametoa wito kwa wanasiasa wa upinzani kuacha zoezi hilo lianze, huku akiwaomba kuketi kwenye meza ya mazungumzo ili kutafutia ufumbuzi wa suala hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.