Pata taarifa kuu
LIBYA-SUDANI-Mapigano-Usalama

Libya: mdororo wa usalama watia hofu majirani

Nchi ya Sudan imesema inaandaa mkutano wa majirani wa Libya utakao fanyika Desemba 4, wakati nchi hiyo ya Afrika Kaskazini ikiendelea kukabiliwa na uasi na vurugu.

Rais wa Sudani, Omar Al bashir, akisema kutiwa hofu na hali inayojiri wakati huu Libya.
Rais wa Sudani, Omar Al bashir, akisema kutiwa hofu na hali inayojiri wakati huu Libya. (Photo : AFP/Isam Al-Haj)
Matangazo ya kibiashara

Mawaziri wa nje wa Algeria, Chad, Misri, Niger na Tunisia wamealikwa kwenye mkutano huo mjini Khartoum pamoja na Katibu mkuu wa Umoja wa nchi za Kiarabu Nabil al-Arabi na balozi wa umoja huo nchini Libya, Nasser al-Qidwa, wizara ya mambo ya kigeni imesema.

Waziri wa mambo ya kigeni wa Sudani Ali al-Karti aliitembelea Libya wiki hii kujadili mkutano huo wa Khartoum na vyama pinzani.

Hayo yakijiri mabomu mawili yaliyotegwa ndani ya gari yamelipuka karibu na balozi zilizofungwa za Misri na Umoja wa Falme za Kiarabu katika eneo linalodhibitiwa na wanamgambo nchini Libya afisa wa Umoja wa Falme za Kiarabu amesema.

Walinzi wawili waliokuwa nje ya jengo la ofisi za ubalozi wa Misri wamejeruhiwa katika mlipuko wa kwanza, shirika la habari la Libya LANA limearifu, huku walinzi wengine watatu wa Umoja wa Falme za Kiarabu pia wakijeruhiwa katika mlipuko wa pili afisa mwandamizi ameliambia shirika la habari la Ufaransa AFP mjini Abudhabi.

Serikali zote mbili za Misri na Falme za Kiarabu zinachukuliwa kama mahasimu wa wanamgambo wa Kiislam ambao waliuteka mji wa Tripoli mwezi Agosti katika mashambulizi ambayo ndege za kivita za Umoja wa Falme za Kiarabu ziliendesha dhidi ngome za wapiganaji wa kiislam, zikitokea nchi jirani ya Misri.

Mapigano kati ya makundi yenye silaha katika eneo muhimu la Qaqaa, mjini Tripoli, Agosti 24 mwaka 2014.
Mapigano kati ya makundi yenye silaha katika eneo muhimu la Qaqaa, mjini Tripoli, Agosti 24 mwaka 2014. REUTERS/Stringer

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.