Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-Katiba-Siasa

Burkina Faso: mtafaruku watokea vurugu

Hali ya utulivu imerejea tangu Alhamisi jioni Oktoba 30 katika mji mkuu wa Burkina Faso, Ouagadougou, baada ya kutokea machafuko yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 20 na wengine wengi kujeruhiwa.

Msemaji wa jeshi la Burkina Faso, akizungumza na waandamanaji kwenye makao makuu ya jeshi, Oktoba 30 mwaka 2014.
Msemaji wa jeshi la Burkina Faso, akizungumza na waandamanaji kwenye makao makuu ya jeshi, Oktoba 30 mwaka 2014. REUTERS/Joe Penney
Matangazo ya kibiashara

Hata hivo ni vigumu kujua idadi sahihi ya watu walifariki katika vurugu hizo, kwani machafuko yalitokea nchi nzima.

Hali ya wasi wasi iliripotiwa Alhamisi jioni Oktoba 30, baada ya kutangazwa kuwa serikali na Bunge vimevunjwa, huku rais akitangaza kuwa hataondoka madarakani wakati ambapo jeshi likitangaza serikali ya “mpito”.

Vurugu hizo zilisababishwa na makabiliano kati ya vikosi vya usalama na waandamanaji ambao waliingia barabarani wakipinga uwezekano wa kuifanyia marekebisho Katiba ya taifa la Burkina Faso, baada ya serikali kutuma muswada wa sheria uhusuo marekebisho ya Katiba, ambao ungelijadiliwa na wabunge Alhamisi Oktoba 30 na baadaye kupitishwa au kupingwa.

Lakini kulikua na uwezekano muswada huo kupitishwa kwani chama madarakani kikiungwa mkono na vyama vingine vilikua na wabunge wengi ambao wangelliweza kuupitisha. Lengo la marekebisho hayo ilikua kumpa nafasi rais Blaise Compaoré ili aweze kugombea kwa muhula mwengine, baada ya kuiongoza nchi hiyo kwa muda wa miaka 27.

Ofisi ya manispa ya jiji na makao makuu ya chama cha CDP vilichomwa moto katika mji wa Bobo Dioulaso, ambao ni mji wa pili nchini Burkina Faso. Kwa mujibu wa mwalimu wa shule ya sekondari akihojiwa na RFI katika mji huo, vurugu ziliyotokea katika mji huo wa Bobo Dioulaso zilisababisha vifo vya watu watano.

Wanajeshi walishikamana na raia waliyokua wakiandamana baada ya jeshi kutangaza kwamba limeivunja serikali na Bunge, jambo ambalo lilishangaza wengi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.