Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-SIASA

Burkina Faso: upinzani waahadi kuendelea na mapambano

Baada ya miezi kadhaa ya maandamano katika mitaa na katika viwanja vya michezo, chama tawala na upinzani wote walikuwa wakisubiri uamuzi wa rais Blaise Compaoré juu ya nini kitatokea kwa ibara ya 37 ya Katiba.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Serikali imeandaa muswada ambao utawasilishwa Bungeni ili upitishwe kwa minajili ya kuitishwa kura ya maoni kuamua iwapo kunahitajika kuongeza au kupunguza idadi ya mihula ya rais kuwa madarakani.

Kila upande ikiwa ni pamoja na chama tawala na upinzani, wamejianda kwa mchakato huo.

Rais Blaise Compaoré ametimiza miaka 27 akiwa madarakani, wakati ambapo Katiba ya nchi ya Burkina Faso haimruhusu kugombea kwa mara nyingine katika uchaguzi wa rais.

Baraza la mawaziri limekutana leo Jumanne Oktoba 21 ambapo limepitisha mswada wa sheria kuhusu marekebisho ya Katiba, mswada ambao utatumwa Bungeni kwa minajili ya kuitishwa kwa kura ya maoni.

“ Baraza la mawaziri limepitisha kwa pamoja mswada wa sheria kuhusu marekebisho ya Katiba ambao utatumwa Bungeni, kulingana na Ibara 163 ya Katiba kwa minajili ya kuitishwa kwa kura ya maoni", Baraza la mawaziri limetangaza.

Muswada huo iwapo utapitshwa, utamuwezesha rais Blaise Compaoré kuitisha kura ya maoni kulingana na Ibara ya 37 ya Katiba.

Kwa upande wake, kiongozi wa chama kimoja cha upinzani, Benewende Stanislas Sankara, amesema hashangazwi na jambo hilo.

" Baada ya kuonekana kuwa mazungumzo ya kisiasa yameshindikana, Tunaweza kusema kwamba kulikuwa na mpango wa siri uliyokua umeandaliwa na rais Blaise Compaoré", amesema Stanislas Sankara.

Chama tawala cha Blaise Compaoré kina wabunge 70, wakati ambapo kunahitajika kura 64 ili mswada huo upitishwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.