Pata taarifa kuu
Afrika Magharibi - Ebola

Watu elfu nne wapoteza maisha Afrika Magharibi kutokana na Janga la Ebola

Idadi ya vifo vilivyotokana na kuzuka kwa maradhi ya ebola katika mataifa ya Afrika magharibi imeongozeka na kufikia zaidi ya watu elfu nne ,shirika la afya la kimataifa WHO limeeleza.

Maradhi ya Ebola yamegharimu takribani maisha ya watu elfu nne Afrika Magharibi
Maradhi ya Ebola yamegharimu takribani maisha ya watu elfu nne Afrika Magharibi REUTERS/Tami Chappell
Matangazo ya kibiashara

Idadi hiyo ya sasa inaonesha vimethibitishwa katika mataifa ya afrika magharibi ikiwemo Guinea, Liberia na Sierra Leone.

Vifo nane vinahusishwa na homa hiyo ya ebola nchini Nigeria na mtu mmoja aliyefariki Marekani.

Kwa ujumla vifo 8,399 vimethibitishwa au kukisiwa hasa katika mataifa ya afrika magharibi.

Katika hatua ya kushangaza, kwa mara ya kwanza mkurugenzi wa shirika la fedha duniani IMF, Christine Lagarde, amesema kuwa shirika lake linalazimika kuachana na sera ya awali ya kutofadhili miradi ya afya na badala yake litatoa fedha kusaidia kukabiliana na kuenea kwa virusi vya Ebola.

Wataalamu wa Afya wa Marekani wameonya kuhusu kuendelea kuenea kwa kasi kwa virusi vya Ebola na kudai kuwa iwapo hautadhibitiwa mapema huenda ukawa janga kubwa zaidi kuliko hata lile la maradhi ya virusi vinavyoambukiza ugonjwa wa UKIMWI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.