Pata taarifa kuu
UN - AFYA

Umoja wa Mataifa wazindua mpango mpya wa kuzuia kusambaa kwa virusi vya Ebola

Umoja wa Mataifa umezindua mpango wa kuzuia kusambaa kwa virusi vya Ebola duniani, wakati huu Guinea, Liberia na Sie re leon zikiendelea kukabiliana na ongezeko la maambukizi.

Matangazo ya kibiashara

Mkuu wa tume ya Umoja wa Mataifa inayoshughulikia Ebola, Anthony Banbury amezindua mpango huo baada ya kuanza ziara ya mataifa ya Afrika Magharibi yaliyoathiriwa na ugonjwa huo hatari.

Banbury amekuwa jijini Monrovia nchini Liberia na kueleza mpango huo wa Umoja wa Mataifa ni pamoja na utoaji wa elimu kuhusu namna ya kuzuia maambukizi na kutoa vifaa kama magari kusaidia kuwasafrisha watu walioambukizwa Ebola hadi katika vituo maalum vya afya.

Wakati hayo yakijiri, dakatri raia wa Uganda aliyekuwa anatoa huduma za kiafya nchini Sierra Leone ameambukizwa Ebola na kusafirishwa Ujerumani kupata matibabu zaidi.
Huu ndio mgonjwa wa pili kutoka Afrika Magharibi kusafirishwa mjini Hamburg nchini Ujerumani kutibiwa.

Wakati uo huo, Marekani inamsafirisha raia wake nyumbani kupata matibabu zaidi ya kuabukizwa Ebola akiwa kazini nchini Liberia.

Mtu huyo ametambuliwa kama Ashoka Mukpo mwanahabari wa kituo cha NBC nchini Marekani.

Shirika la afya duniani, WHO linasema kuwa watu zaidi ya watu elfu tatu wamefariki dunia kutokana na maambukizi ya Ebola nchini Sierra Leone, Liberia na Guinea tangu mapema mwaka huu.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.