Pata taarifa kuu
LIBERIA

Daktari Mkuu nchini Liberia ajitenga na watu baada ya naibu wake kufariki

Daktari Mkuu nchini Liberia ameamua kujitenga na watu kwa siku 21 baada ya naibu wake kufariki kutokana na ugonjwa hatari wa Ebola.

Wataalam wa afya nchini Liberia
Wataalam wa afya nchini Liberia RFI/ Olivier Rogez
Matangazo ya kibiashara

Naibu Waziri wa afya nchini humo Bernice Dahn, amethibitisha kujitenga na daktari huyo wa kike  licha ya kutoonyesha dalili zozote za kuwa na Ebola.

Raia wa Liberia akichukua tahadhari dhidi ya Ebola
Raia wa Liberia akichukua tahadhari dhidi ya Ebola RFI/ Olivier Rogez

Liberia inasalia nchi iliyoathiriwa mno na maambukizi ya Ebola miongoni mwa nchi za Afrika Magharibi na kulingana na takwimu za Shirika la afya duniani  WHO, watu zaidi 1,800  wamepoteza maisha nchini Liberia pekee hadi sasa.

Nchi zingine zilizoathiriwa na Ebola ni pamoja na Guinea na Sierra Leone.

Mhudumu wa afya nchini Liberia
Mhudumu wa afya nchini Liberia RFI/ Olivier Rogez

WHO imeonya kuwa ikiwa hali itaendelea kuwa hivi, watu zaidi ya elfu 20 wataambukiwa Ebola katika nchi hizo kufikia mwezi Novemba.

Wahudumu wa afya nchini Liberia
Wahudumu wa afya nchini Liberia RFI/ Olivier Rogez

Marekani imetuma wanajeshi wake 3,000 nchini Liberia kusaidia kupambana na ugonjwa huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.