Pata taarifa kuu
DRC-Siasa

DRC: wabunge kutoka upinzani watishia kususia vikao vya Bunge

Wabunge kutoka vyama vya upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na waanowakilisha vyama kadhaa wametangaza nia yao ya kususia mijadala ya Bunge inayoendelea kuhusu marekebisho ya katiba.

Etienne Tshisekedi (kushoto) pamoja na Vital Kamerhé (kulia), viongozi wawili wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Etienne Tshisekedi (kushoto) pamoja na Vital Kamerhé (kulia), viongozi wawili wa upinzani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. AFP/ Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Chama cha pili cha upinzani kwa ukubwa nchini humo cha UNC cha bwana Vital Kamerhe na chama kikuu cha upinzani cha UDPS cha Etienne Tshisekedi bado baadhi ya wabunge wao wanaendelea kuwepo bungeni, huku wawakilishi wao katika tume huru ya uchaguzi wakiwa tayari wamejiondoa katika tume hiyo.

Madhumuni ya hatua hiyo kwa muda ni kuishinikiza serikali ya kinshasa kuachana na mpango wake wa kurekebisha katiba na kutaka mazungumzo ya kina na serikali hiyo, kama alivyobainisha Vital Kamerhe mwenyekiti wa chama cha upinzani cha UNC nchini DRC.

Katika hatua nyingine mashirika ya kiraia yameunga mkono tamko la maaskofu nchini drc kuhusiana na mabadiliko ya katiba yanayotarajiwa kufanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.