Pata taarifa kuu
UN-WATOTO

Mtoto 1 kati ya 10 hudhalilishwa kingono duniani: UN

Inakadiriwa kuwa wasichana milioni mia moja na ishirini duniani, mmoja kati ya wasichana kumi aidha amebakwa au kudhalilishwa kingono wanapofikia umri wa miaka 20, ripoti mpya ya Umoja wa mataifa imesema. 

Moja ya watoto nchini India walioandamana hivi karibuni kupinga vitendo vya ubakaji
Moja ya watoto nchini India walioandamana hivi karibuni kupinga vitendo vya ubakaji Reuters
Matangazo ya kibiashara

Hii ni kwa mujibu wa takwimu mpya zilizokusanywa toka nchi mia moja na tisini duniani, ambapo utafiti wake unaelezwa kuwa mkubwa zaidi kuwahi kufanywa kuhusu unyanyasaji wanaofanyiwa watoto.

Ripoti hii iliyopewa jina la “Hidden in Plain Sight” pia imebainisha kuwa moja ya tano ya watu wote waliouawa, wengi ni watoto na vijana, huku matukio ya kujiua yakishamiri hasa kwa vijana wakiume kwenye bara la Amerika zikiwemo nchi za Venezuela, Colombia, Panama na Brazil.

Mkurugenzi wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na watoto, UNICEF, Anthony Lake anasema “takwimu hizi zinaogofya, na hakuna Serikali wala mzazi ambaye angependa kuona haya” alisema Lake.

Ripoti hiyo imedai kuwa vitendo vya udhalilishaji wa ngono dhidi ya wasichana vimekithiri na kuonya kuwa iwapo hatua za haraka hazitachukuliwa dunia itapoteza nguvu kazi na viongozi wanawake wa baadae.

Ripoti hii pia imeeleza kuwa wengi wa watoto ambao wameshawahi kufanyiwa vitendo hivo aidha wameshajiua ama wengi wao huishia kutoa uhai wao jambo ambalo linaogopesha zaidi.

Zaidi rpoti hii imeonesha kuwa athari za afya kiakili ikiwemo msongo wa mawazo, jazba, matamanio na ndoto za kutisha ni miongoni mwa matatizo ambayo yanawaandamana wasichana na vijana ambao wamewahi kufanyiwa vitendo hivi.

UNICEF imeonya pia kuhusu matumizi ya mtandao kwa watoto katika dunia ya leo, kuwa ni sehemu ya chanzo na sababu inayopelekea kukithiri kwa vitendo vya udhalilishaji wa ngono kwa watoto.

UNICEF inadai kuwa watoto wanaona ni rahisi zaidi kubadilishana taarifa kwenye mtandao kuliko sehemu nyingine yoyote, lakini hawajui kwakufanya hivyo wanajiweka kwenye hali hatarishi ikiwa ni pamoja na kusakwa na watu wanaoshiriki kutekeleza vitendo hivi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.