Pata taarifa kuu
UN- UKANDA WA MAZIWA MAKUU-Uteuzi

UN : Said Djinnit mwakilishi mpya wa Ban Ki- Moon katika ukanda wa Maziwa makuu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-Moon, amemteua Said Djinnit wa Algeria kuwa Mjumbe wake katika Ukanda wa Maziwa Makuu.

Saïd Djinnit, mwakilishi mpya wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Saïd Djinnit, mwakilishi mpya wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Maziwa Makuu. AFP/SEYLLOU
Matangazo ya kibiashara

Saïd Djinnit , mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Afrika ya magharibi ameteuliwa kuwa mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Maziwa Makuu.
Saïd Djinnit , mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Afrika ya magharibi ameteuliwa kuwa mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa katika ukanda wa Maziwa Makuu. africa-union.org

Bwana Djinnit anaichukua nafasi ya Bi. Mary Robinson wa Ireland, ambaye amekubali wadhifa mpya aliopewa na Katibu Mkuu kama Mjumbe wake kuhusu mabadiliko ya tabianchi.

Mary Robinson aliekua mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa.
Mary Robinson aliekua mwakilishi wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa. AFP PHOTO/JUSTIN TALLIS

Kuanzia mwaka 2008 hadi hivi karibuni, Bwana Djinnit amekuwa Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Msimamizi wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Afrika ya Magharibi.

Bwana Djinnit pia amehudumu kama Mwakilishi wa ngazi ya juu wa Katibu Mkuu nchini Nigeria, katika kusaidia juhudi za kupambana na kundi la wapiganaji la Boko Haram.

Djinnit ana uzeofu mkubwa katika masuala ya diplomasia, akiwa amewahi kuhudumu kama Kamishna wa Usalama na Amani wa kwanza wa Muungano wa Afrika, AU, na kama Msaidizi wa Katibu Mkuu wa masuala ya kisiasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.