Pata taarifa kuu
UGANDA

Marekani imeiwekea vikwazo Nchi ya Uganda.

Serikali ya Marekani imeiwekea vikwazo nchi ya Uganda kama adhabu kwa kupitisha sheria dhidi ya ushoga ambayo imelinganishwa na Waziri John Kerry kuwa sawa na sheria ya Nazi nchini Ujerumani au ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry wakati wa ziara yake London Uingereza June 13, 2014
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry wakati wa ziara yake London Uingereza June 13, 2014 REUTERS/Luke MacGregor
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo mpya iliidhinishwa na rais Yoweri Museveni mwezi februari mwaka huu na kukashifiwa na mataifa ya magharibi yakiongozwa na Marekani ambayo yanasema ni sheria inayokiuka haki za binadamu nchini humo.

Vikwazo vilivyotangazwa na Marekani ni pamoja na kuwanyima visa vya kusafiri nchini Marekani baadhi ya viongozi wa serikali ya Kampala, ambao wamekuwa katika mstari wa mbele kuuunga mkono kupitshwa kwa sheria hiyo.

Aidha, Marekani inasema inasitsiha ufadhili wa kIfedha katika idara ya polisi, Wizara ya afya na kutoa mafuzno ya jeshi la angaa kwa taifa hilo la Afrika Mashariki.

Hata hivyo, Marekani imeweka wazi kuwa itaendelea kushirikiana na Uganda katika juhudi za kumsaka kiongozi wa kundi la waasi la LRA Joseph Kony .

Serikali ya Uganda imekuwa ikisisitiza kuwa haitishwi na vikwazo kutoka nchi za Magharibi na lengo kuunda sheria ya kupinga mapenzi ya jinsia moja ni kudumisha mila na desturi za kiafrika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.