Pata taarifa kuu
RWANDA

Mwandishi wa Habari wa gazeti Umurabyo la Rwanda aachiwa huru.

Mwandishi wa habari wa Rwanda Agnes Uwimana Nkusi ameachiwa huru jana baada ya kutumikia kifungo cha muda wa miaka minne jela kwa kumkosoa Rais Paul Kagame katika makala yake.Alipoachiwa huru, Agnes Nkusi ameelezea furaha yake na azma yake ya kuendelea na jukumu la kuhabarisha umma wa Rwanda na kuwa hana hofu ya aina yoyte wala hajutii kilichomtokea pamoja na utayari wake kufanya ya uandishi wa habari hadi kufa kwake.

Agnes Uwimana Nkusi (Kushoto) na Saidati Mukakibibi (katikati), wawili hawa ni wanahabari wakiwa katika mavazi ya wafungwa, Kigali Rwanda. January 30 2012.
Agnes Uwimana Nkusi (Kushoto) na Saidati Mukakibibi (katikati), wawili hawa ni wanahabari wakiwa katika mavazi ya wafungwa, Kigali Rwanda. January 30 2012. AFP/Steve Terrill
Matangazo ya kibiashara

Mhariri huyo wa gazeti “Umurabyo” alikamatwa tarehe 8 mwezi Julai mwaka 2010 na kuhukumiwa kufungo cha miaka 17 jela kwa kosa la kuchochea uvunjaji wa sheria na kukana mauaji ya kimbari dhidi ya Watutsi wa Rwanda mwaka 1994.

Alipunguziwa adhabu yake hadi miaka minne jela kwa kuhatarisha usalama wa taifa, baada ya majaji kukosa ushahidi kuhusu tuhuma zilizomkabili mwanahabari huyo.

Shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty International na lile la kutetea haki za Waandishi wa habari Wasiokuwa na Mipaka (RSF) wamelaani kifungo cha mwandishi wa habari huyo na katika taarifa yake, shirika la RSF limeridhishwa na hatua ya kutolewa gerezani kwa Bi Nkusi.

Nchi ya Rwanda imeorodheshwa na shirika la RSF kuwa kwenye nafasi ya 162 kati ya nchi 180 duniani katika kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari, taarifa iliyotolewa mwaka huu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.