Pata taarifa kuu
MISRI

Sisi atangazwa rasmi mshindi wa uchaguzi nchini Misri, awataka wananchi kudumisha amani na usalama

Aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Misri, Jenerali Abdel Fattah al-Sisi hapo jana ametangazwa rasmi na tume ya taifa ya uchaguzi kama mshindi kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika juma moja lililopita akipata asilimia 96.9 ya kura zote. 

Rais mteule wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi
Rais mteule wa Misri, Abdel Fattah al-Sisi REUTERS/Maxim Shemetov
Matangazo ya kibiashara

Uchaguzi huo uliofanyika juma moja lililopita ulilazimika kufanyika kwa siku tatu zaidi kuhofia idadi ndogo ya watu kujitokeza kupiga kura, ambapo mwenyekiti wa tume ya taifa ya uchaguzi nchini humo, Anwar Rashad al-Asi amesema asilimia 47.45 ya watu walijitokeza.

Ushindi wa Al-Sisi ulitarajiwa na wananchi wengi wa Misri ambao wengi bado wanamuona Jenerali huyu kama shujaa wao baada ya kuiangusha Serikali ya Mohamed Morsi mwezi July mwaka uliopita.

Matokeo haya ya uchaguzi yameonesha kuwa mpinzani wa Al-Sisi kwenye uchaguzi huo alipata asilimia 3 pekee ya kura zote ambazo zilihesabiwa, kura ambazo hata yeye mwenyewe amekubalia kushindwa.

Jenerali, Abdel Fattah al-Sisi
Jenerali, Abdel Fattah al-Sisi REUTERS/Jamal Saidi

Mfalme wa Saudi Arabia, Mfalme Abdullah ambaye alikuwa mpinzani mkubwa wa Serikali ya Morsi, ameitisha haraka mkutano wa wafadhili kuisaidia nchi ya Misri saa chache baada ya matokeo hayo kutangazwa.

Baada ya matokeo hayo kutangazwa, Jenerali al-Sisi alitoa wito kwa wananchi wa taifa lake kufanya kazi kwa nguvu na kuhakikisha wanalinda usalama wa nchi yao na kujishughulisha kwenye shughuli za kiuchumi ili kusimamisha tena uchumi wa taifa hilo.

Wafuasi wa Jenerali al-Sisi
Wafuasi wa Jenerali al-Sisi REUTERS/Asmaa Waguih

Rais al-Sisi anasema "Matarajio yetu yako kwenye ukurasa mtupu, na nijukumu ambalo liko kwenye mikono yetu kulifanikisha na kufanya tunachotaka, kupata mkate, uhuru, utu na utawala wa Sheria". alisema al-Sisi.

Licha ya wananchi wengi kuonesha kuwa na imani na utawala wa al-Sisi baadahi ya wanaharakati na wanasiasa wa upinzani nchini Misri bado wanaonesha hofu kuhusu utawala wake na kwamba huenda akaweka sheria kali zaidi ambazo zitaminya uhuru wa watu kutoa maoni.

Inakadiriwa kuwa zaidi ya watu 1400 wengi wao wakiwa ni kutoka madhehebu ya kiislamu na chama cha Muslim Brotherhood wameuawa huku wengine zaidi ya 1500 wanashikiliwa na polisi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.