Pata taarifa kuu
MALAWI-Siasa-Uchaguzi

Mahakama Kuu ya Malawi yapinga hatua ya raisi Banda kubatilisha uchaguzi

Mahakama Kuu nchini Malawi imepinga uamuzi wa rais Joyce Banda kutengua uchaguzi mkuu uliofanyika juma lililopita wiki hii - ambao yeye alikuwa miongoni mwa wagombea.

Mahakama nchini Malawi yapinga maamuzi ya raisi Banda kubatilisha uchaguzi
Mahakama nchini Malawi yapinga maamuzi ya raisi Banda kubatilisha uchaguzi
Matangazo ya kibiashara

Bi Banda hapo awali alisema uchaguzi wa siku ya Jumanne uligubikwa na wizi wa kura na kutangaza uchaguzi mwingine kufanyika ndani ya siku 90 zijazo na bila yeye kugombea.

Hata hivyo hatua hivyo imepingwa vikali na mkuu wa tume ya uchaguzi ambaye amesema raisi hana mamlaka ya kutengua uchaguzi huo.

Aidha mahakama kuu ya Malawi ikafanya maamuzi yake baada ya tume ya uchaguzi kusema mbali ya changamoto zilizojitokeza bado kura zinahesabiwa na kura zilizohesabiwa ni halali.

Raisi Banda alitangaza hayo kupitia kituo cha Radio moja nchini humo na kusema kwa mamlaka aliyonayo kikatiba anatangaza kuwa uchaguzi huo ni batili.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.