Pata taarifa kuu
MALAWI-Uchaguzi

Malawi: Mahakama Kuu yaamuru yatangazwe matokeo ya uchaguzi

Mahakama kuu nchini Malawi imeruhusu yatangazwe matokeo ya uchaguzi mkuu wa urais, wabunge na madiwani, baada ya rais anaeondoka madarakani Joyce Banda kufikisha malalamiko yake kwenye mahakama hio, akibaini kwamba uchaguzi uligubikwa na wizi wa kura.

Raia wakisubiri kushiriki katika zoezi la kupiga kura, nchini Malawi, Mei 20 mwaka 2014.
Raia wakisubiri kushiriki katika zoezi la kupiga kura, nchini Malawi, Mei 20 mwaka 2014. afp.com/Gianluigi Guercia
Matangazo ya kibiashara

“Matokeo yamekua yakiwasili kwa mwendo wa kinyonga lakini, baada ya zoezi la uhesabuji wa kura kumalizika, na kwa sasa tuna asilimia 12 ya jumla ya matokeo”, amesema mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, Maxon Mbendera, akibaini kwamba anajiandaa kutangaza matokeo ya mwanzo iwapo matokeo yatakua yamefikia asilimia 30.

Tume ya uchaguzi ilikabiliwa jana alhamisi na tatizo la kiufundi baada ya mitambo ya kielektroniki iliyokua ikihesabu kura kusimama kwa muda, lakini tume hio imekanusha habari zisemazo kwamba kulikueko na njama za kuiba kura. Mwenyekiti wa tume hio, ameahidi kutangaza matokeo ya kweli na uhakika bila kuegemea upande wowote.

“Hatutashurutishwa kutangaza haraka matokeo ya uchaguzi. Tumetaka tu kutuliza nyoyo wananchi kwamba tutatangza matokeo ya ukweli na uhakika, na tutarekebisha kasoro zote ziliyojitikeza katika uchaguzi huo, kwani tumeshapata mashitaka 135”, amesema Maxon Mbendera.

Baada ya kuwa na wasiwasi na zoezi hilo la uchaguzi,hapo jana alhamisi chama cha rais anaeondoka madarakani Joyce Banda (PP), kilifikisha malalamiko yake kwenye Mahakama kuu na kuomba matokeo yasitangazwi na zoezi la uhesabuji lirejelewe

Chama cha PP kimesema kwamba matokeo yaliyotolewa katika baadhi ya mikoa hayaambatani na idadi ya wapiga kura ya vituo mbalimbali vya kupigia kura, kikihisi kwamba mitambo ya kielektroniki iliyotumiwa kwa kuhesabu kura imechezewa.

Lakini jaji Mike Temboametupilia mbali tuhuma hizo akibaini kwamba matokeo rasmi hayajatolewa.

Matokeo ya awali yaliyotangazwa na vyombo vya habari vya Malawi yanaonyesha kuwa rais Joyce Banda ameshindwa katikauchaguzi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.