Pata taarifa kuu
JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI

Viongozi wa Jumuia ya Afrika Mashariki wakutana

Viongozi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wamekutana leo mjini Arusha Tanzania kuzungumzia maswala muhimu kuhusu jumuiya hiyo. Miongoni mwa maswala yaliyoyojadliwa katika mkutano wa viongozi hao ni pamoja na kutathmini ombi la Sudan Kusini kujiunga na Jumuiya hiyo. 

Rais wa Kenya, akiwa pia mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uhuru Kenyatta.
Rais wa Kenya, akiwa pia mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Uhuru Kenyatta. REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambaye pia ni rais wa Kenya Uhuru Kenyatta ametoa wito kwa nchi wananchi kutekeleza maazimio yaliyokubaliwa katika miaka iliyopita ili kuimarisha jumuiya hiyo.

Akizungumza katika Mkutano wa viongozi wa Jumuiya hiyo mjini Arusha Tanzania makao makuu ya jumuiya hiyo, rais Kenyatta amesisitiza kuwa makubaliano ya yaliafikiwa ya matumzi ya sarafu moja mwaka uliopita ni mwanzo wa mafanikio ya jumuiiya hiyo na wananchi wa mataifa hayo kutengamana kwa urahisi .

Kuhusu mzozo wa Sudan Kusini, rais Kenyatta amesema kuwa Jumuiya hiyo itafanya kila kilicho ndani ya uwezo wake kusaidia kurejesha amani, lakini ametoa wito kwa pande mbili zinazozazana kuacha vita na kukubaliana.

Sudan Kusini iliomba kujiunga na Jumuiya ya Afrika Mashariki pindi tu ilipopata uhuru wake mwaka 2011, lakini viongozi hao wamechelewesha kuiruhusu Juba kwa kile walichosema nchi hiyo changa bado haijashuhudia utulivu na uchumi wake bado ni mdogo.

Mazungumzo ya kujadili ombi la Sudan Kusini kujiunga kama mwanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki yameahirishwa hadi mwezi septemba mwaka huu. Mbali na rais Kenyatta viongozi wengine waliohudhuria mkutano huo ni pamja na rais wa Tanzania Jakaya Kikwete, rais Uganda Yoweri Museveni, Makamu wa rais wa Burundi Prosper Bazombanza na waziri Mkuu wa Rwanda Pierre Damien Habumuremyi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.