Pata taarifa kuu
SUDANI KUSINI-Sheria

Waasi wa Sudani Kusini: wakaribia kuliteka eneo lenye mafuta

Sudani kusini inaendelea kukumbwa na vita vya wenyewe kwa wenyewe, huku Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na jumuiya ya kimataifa , vikitishia kuchukua vikwazo, baada ya mamia ya raia kuuawa katikati ya mwezi wa aprili.

Salva Kiir, rais wa Sudani Kusini, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Juba.
Salva Kiir, rais wa Sudani Kusini, katika mkutano na waandishi wa habari mjini Juba. REUTERS/Andreea Campeanu
Matangazo ya kibiashara

Wakati huohuo waasi wamebaini kwamba wamevikaribia visima vya mafuta kaskazini mashariki mwa taifa hilo changa, eneo ambalo limeathirika na mapigano ya hivi karibuni. Hali hio ya kupoteza baadhi ya maeneo, hasa mji wa Bentiu, kulipelekea rais wa Sudani Kusini Salva Kiir anachukua uamzi wa kumfuta kazi mkuu wa majeshi.

Hayo yakijiri waziri wa sheria nchini Sudani Kusini, amefahamisha kuwa ameomba vyombo vya sheria nchini humo kufuta kesi dhidi ya washukiwa wanne wa jaribio la mapinduzi na ambao wanachukuliwa kuwa watu wa karibu na Riek Machar aliyechukuwa uongozi wa uasi tangu mwezi desemba mwaka jana.

Waziri Paulion Wanawilla amesema ili kutia kipao mbele swala la mazungumzo, maridhiano na uwiano baina ya wananchi wa Sudani Kusini, ameamuru kufuta kesi dhidi ya watuhumiwa hao wanne na ambao wataachiwa huru hii leo.

Kesi dhidi ya watuhumiwa wengine saba walioacha huru na kukabidhiwa serikali ya kenya mwishoni mwa mwezi januari iliopita nayo pia inatakiwa kufutwa.

Makamu wa zamani wa rais Salva Kiir, Riek Machar katika jimbo la Jonglei, nchini Sudani Kusini,januari 31 mwaka 2014.
Makamu wa zamani wa rais Salva Kiir, Riek Machar katika jimbo la Jonglei, nchini Sudani Kusini,januari 31 mwaka 2014. REUTERS/Goran Tomasevic

Hata hivo, waziri huyo amesema kesi ambayo bado haijafutwa ni ile inayomkabili Riek Mashar na watu wake wengine wawili ambao ni Taban Deng Gai gavana wa zamani wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Unity na Alfred Lado Gore waziri wa zamani wa mazingira na alikuwa mshauri wa rais Salva Kiir ambao ni viongozi waliopambana katika harakati za ukombozi wa taifa hilo na ambo wote wapo mafichoni.

Kesi dhidi ya wajumbe hao wanne ambao ni Pagan Amum katibu mkuu wa chama madarakani cha SPLM Oyai Deng Ajak waziri wa zamani wa usalama, Ezekiel Lol Gatkuoh balozi wa zamani wa Sudani Kusini jijini Washington, pamoja na Majak D'Agoot naibu waziri wa ulinzi, ilizinduliwa tangu mwezi March iliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.