Pata taarifa kuu
Mauritania-Maandamano

Mtu mmoja apoteza maisha katika maandamo ya waislam jijini Nuakchott kupinga kitendo cha kuchanwa kwa Koran

Mtu mmoja ameuawa nchini Mauritania na wengine wamejeruhiwa wakati wa maandamano ya waislam waliokuwa wakionyesha ghadhabu baada ya kueneea kwa taarifa za kuchanwa kwa kitabu kitakatifu Koran katika mji mkuu Nouarkchot na mtu asiyejulikana.

Maandamano jijini Nouakchott
Maandamano jijini Nouakchott
Matangazo ya kibiashara

Imamu mmoja aliripoti tukio la wanaume wanne waliofunika nyuso kwa vilemba waliingia msikitini na kuchana kurasa za Koran na kuzitupa chooni.

Msemaji wa serikali ya Mauritania Sidi Mohamed Ould Maham amesema aliyeuawa ni mwanafunzi wa chuo kikuu na hajauawa kwa risase, na tayari uchunguzi umeanzishwa ili kujuwa ukweli kuhusu tukio hilo.

Polisi walitumia nguvu na mabomu ya kutowa machozi katika kuwatawanya waandamanaji jijini Nouakchott wakati waislam walikusanyika mjini hapa wakiandamana kuelekea ikulu ya rais.

Waandamanaji hao walikuwa wakitamka Allahou akbar, ikimaanisha Mungu ni mkubwa, na auawe muhusika wa kukidhihaki kitabu kitakatifu. Miongoni mwa waandamanaji hao walitiwa nguvuni huku wengine wakijeruhiwa.

Maandamano mengine yaliandaliwa katika maeneo mbalimbali ya nchi hususan katika miji ya Kiffa na Aioun kusini mashariki mwa nchi hiyo.

Msemaji wa serikali Oul Maham amewatolea wito waislam nchini humo kujizuia kuanguka katika mtego wa watu ambao wanania ya kucheza na hisia za waislam kwa faida zao binafsi.

Uchunguzi umeanzishwa kubaini tukio hilo la kuchanwa kwa kitabu kitakatifu ambacho ni Koran na wahusika watakamatwa, amesema msemaji huyo wa serikali huku akilaani kitendo hicho dhidi ya hisia za wananchi wa Mauritania ambao ni waislam na wanaheshimu maadili yake.

Maandamano hayo ya jana yanakuja baada ya mengine yaliokuwa yameandaliwa juzi Jumapili jijini Nouakchott ambapo ma mia ya waislam wameshiriki kuelekea katika kata ya Teyarett kaskazini mwa mji mkuu hadi Ikulu.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.