Pata taarifa kuu

Rais Kikwete amkabidhi rais Chissano hoja za Tanzania kuhusu mgogoro wa mpaka baina ya Malawi na Tanzania

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete jana Jumatatu amekutana na rais mstaafu wa Msumbiji Joachim Chissano ambaye ni msuluhishi wa mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi kuhusu ziwa Nyasa.

Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete
Rais wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete tanzania
Matangazo ya kibiashara

Rais Chissano na ujumbe wake umo nchini Tanzania kusikiliza hoja zake kuhusu mpaka wa ziwa Nyasa ambapo rais Kikwete tayari amewasilisha hoja za ushahidi kuhusu eneo hilo kwa ujumbe huo.

Hatua hii inajiri baada ya msuluhishi huyo kusikiliza hoja za Malawi ambapo baada ya kusikiliza hoja za nchi zote mbili , hoja hizo zitatafsiriwa  na kuzingatiwa  katika kutafuta suluhu ya mgogoro wa ziwa Nyasa.

Awali kabla ya kupokea ujumbe wa rais Chissano, rais Kikwete alifanya mazungumzo na mjumbe maalum wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa UN kwenye eneo la maziwa makuu Bi Mary Robinson kuhusu maendeleo na jitihada zilizofanywa kuleta amani Mashariki mwa DRCongo ambapo Tanzania imetoa mchango mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.