Pata taarifa kuu
Marekani-uhusiano

Marekani yakiri uhusiano wake na Pakistan kuingia doa kufuatia mashambulizi yake ya ndege zisizokuwa na rubani kwenye ngome za wanamgambo wa Taliban

Serikali ya Marekani kwa mara nyingine tena imekiri kuwa na uhusiano usio mzuri na nchi ya Pakistan kufuatia hatua yake ya kuendelea kutekeleza kwa siri mashambulizi ya ndege zisizo na rubani kwenye maeneo ya wanamgambo wa Taliban.

Ndege zisizokuwa na rubani Drone
Ndege zisizokuwa na rubani Drone
Matangazo ya kibiashara

Kauli ya Ikulu ya Marekani inatolewa wakati huu ambapo hapo jana waziri mkuu wa Pakistan, Nawaz Sharif akionya kuwa amani inaweza isifikiwe nchini humo kati ya nchi yake na wanamgambo wa talibana ikiwa Marekani itaendelea na mashambulizi dhidi ya Taliban.

Waziri mkuu, Sharif, amekosoa mauaji ya kiongozi wa kundi la Taliban nchini Pakistan, Hakimullah Mehsud ambaye aliuawa mwishoni mwa juma lililopita kwenye shambulio la ndege zisizo na rubani kwenye milima ya mpakani na nchi ya Afghanistan.

Kauli ya Sharif, iliungwa mkono na rais wa Afghanistan, Hamid Karzai ambaye amedai kuwa mauaji ya Mehsud yamefanyika wakati ambao haukuwa mzuri kwakuwa tayari jitihada za kusaka muafaka kati ya kundi hilo na serikali zao zilikuwa zimeanza kuzaa matunda.

Mpaka sasa kundi la Taliban halijatangaza hatua ambazo itazichukua kuhusu mazungumzo ya amani, jambo ambalo wachambuzi wa mambo wanaona kuwa mauaji ya Mehsud hayakufanyika wakati muafaka na kwamba huenda kusiwe na suluhu kati yaio na kundi la Taliban.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.