Pata taarifa kuu
DRC

UN kutumia ndege zisizo na rubani kuwashambulia waasi DRC

Umoja wa Mataifa UN umetangaza utaanza kutumia kwa mara ya kwanza ndege za kivita zisizo na rubani katika Jamhuri ya Kidemomkrasia ya Congo katika juhudi za kusambaratisha makundi ya waasi katika eneo.

Matangazo ya kibiashara

Kamanda Mkuu wa Kikosi Maalum cha Umoja wa Mataifa Jenerali Carlos Alberto Dos Santos Cruz amethibitisha mpango huo na kusema watatumia zana za kisasa zaidi katika kuhakikisha wanapambana na waasi waliojirani na Mji wa Goma.

Wakati hayo yakijiri Mkuu wa Kikosi cha Umoja wa Mataifa kinacholinda Amani nchini MONUSCO Martin Kobler wana ushadi kuwa waasi wa M 23 wanaendelea kuimarisha ngime zake Mashariki mwa nchi hiyo.

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto Duniani UNICEF kupitia Mwakilishi wake nchini DRC Barbara Benteme amethibitisha wamezungumza na watoto wengi ambao wanakiri walisajiliwa katika Jeshi la Rwanda.

Umoja wa Mataifa umekuwa katika mstari wa mbele kwa sasa katika kuhakikisha wanakabiliana vilivyo na makundi yanayomiliki silaha yanayopatikana Mashariki mwa DRC kwani yamekuwa yakifubaza usalama wa eneo hilo.

Huku mikakati hiyo ikiendelea, mazungumzo ya amani kati ya waasi hao wa M 23 na wajumbe wa serikali ya DRC yanaendelea jijini Kampala nchini Uganda kwa zaidi ya mwezi mmoja sasa suluhu bado halijafikiwa.

Mapema juma hili, wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa walikuwa Mashariki mwa Goma kuthathmini hali ya usalama katika eneo hilo na baadaye kukutana na marais wa Rwanda na Uganda ambao wameendelea kupinga kuwaunga mkono waasi wa M 23.

Wiki iliyopita, Marekani ilitangaza kuiwekea vikwazo serikali ya Kigali kwa kusitisha kutoa mafunzo ya kijeshi kwa tuhma hizo za kuwaunga waasi hao ambao wanatuhumiwa kuwatumia watoto katika jeshi lake tuhma ambazo wamekanusha.
 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.