Pata taarifa kuu
MISRI-MAHAKAMA

Mohamed Morsi kupandishwa kizimbani kwa tuhuma za mauaji ya waandamanaji

Rais aliyeondolewa madarakani na jeshi la Misri, Mohamed Morsi anatarajiwa kupandishwa kizimbani kusomewa mshataka ya mauaji ya waandamanaji wakati wa utawala wake.

AFP PHOTO/OZAN KOSE
Matangazo ya kibiashara

Televisheni ya Taifa la Misri imeripoti kuwa Mohamed Morsi sanjari na wanachama 14 wa chama cha Muslim Brotherhood watasomewa mashitaka ya mauaji ya waandamanaji nje ya ikulu ya Rais mwezi desemba mwaka jana ingawa haijaweka wazi tarehe ya keshi hiyo kuanza.

Mwezi Desemba mwaka jana maelfu ya waandamanaji walipiga kambi nje ya Ikulu mjini Cairo wakipinga hatua ya Morsi kujiongezea madaraka na kulazimisha upitishwaji wa katiba inayopendelea zaidi upande wa waislam.

Morsi aliyewekwa mafichoni tangu Julai 3 mwaka huu anakabiliwa na mshitaka mengine ya kutoroka gerezani mwaka 2011.

Wimbi la viongozi wa Muslim Brotherhood na wafuasi wao kukamatwa limeendelea kushika kasi, tayari wanachama zaidi ya elfu mbili wanashikiliwa na vyombo vya dola toka Morsi aondolewe madarakani.

Umoja wa Afrika AU umetoa wito kwa wanachama wa Muslim Brotherhood kushirikiana na serikali ya mpito ili kumaliza machafuko yanayoendelea kuligawa Taifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.